Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za viongozi Serikalini Ikulu jijini Dares Salaam, leo tarehe 03 Januari, 2023.

Amesema “Mtakumbuka kuwa Novemba 2022, Bunge la Tanzania lilikuwa na mjadala mzito kidogo kuhusu matumizi ya fedha na madaraka katika ofisi zetu za Kibalozi zilizopo Nchi mbalimbali, Serikali inafanyia kazi kasoro zilizoelezwa ili kurudisha hadhi ya balozi zetu.

“Nimefanya mabadili katika ofisi ya Ubalozi iliyopo New York, ambayo inakuwa na Mwakilishi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.

“Ofisi hii ni muhimu kwa Nchi yetu kwa kuwa ndio inatuwakilisha katika mambo yanayojadiliwa na mataifa na taasisi za kimataifa zilizo chini ya Umoja wa Mataifa Mjini New York.

“Ofisi yetu hiyo inahitaji mwanadiplomasia mahiri anayejua siasa za kimataifa, mzalendo kwa nchi yake na mtulivu wa hekima na busara.

“Hivyo nimeamua kumrudisha nyumbani Prof. Kennedy Gaston aliyeko Ofisi ya New York na kumpeleka Hussein Othman Kattanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

“Kattanga anaenda kuiwakilisha Tanzania kama Balozi wa Kudumu huko New York.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi itajazwa na DKT. Moses Mpogole Kusiluka aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Ikulu itajazwa na Diwani Athuman Msuya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

“Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa itajazwa na Said Hussein Massoro aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za ndani za TISS.”



Watanzania ni wazuri wa kulala na kutokusoma haya yanatokea yalisha semwa 2 years back. Nawengine walisha sema what is next... Keep silence keep pray hujuwi hujuwi ila Mungu ni wetu sote
 
Promotion ya kutoka kuwa Karibu Mkuu kiongozi hadi kuwa balozi Marekani na wa kudumu UN?
KM ndio boss wa mabalozi wote
Nadhani immediate Boss wa Mabalozi ni Katibu Mkuu wizara ya mambo ya nje,ambaye Katibu Mkuu Kiongozi ndie Kiongozi wake...so...ingekua ni ligi ya soka,jamaa kashuka kutoka Daraja la kwanza hadi la tatu...but it is all semantics...yeye na Bashiru bado salary slips zao zinaweza zikawa sawa...
 
Huyu Katanga ndio alikuja kwa staili ya kutengeneza serikali yenye muunganiko na ufanisi katika utendaji wake? Binafsi sikuona mabadiliko chanya yoyote.
Inawezekana Kuna kazi ya kufanya huko UN Kuna vitu may be haviendi sawa,..kwenye Vita always mtapeleka mwanajeshi wenu mahiri..
Kuna dhana moja kua ukifanya vizuri sehemu bas ufie Hapo Hapo hii si sawa wakuu..
Mimi naamimi Kuna assignment balozi kattanga amepewa na mamlaka...
 
Nchi hii kwani hata ikiaribika, ikafilisika, mambo yakawa mabaya wewe utaharibikiwa na nini??
Afta loo wewe si sehemu ya wanaomiliki hii nchi, wewe unadai uzalendo wenzio wanalamba asali??
Uzalendo upi unautaka
Mtajijua wenyewe, mimi mchangiaji tu nilishaondoka huko mwaka wa 45.huu [emoji1] [emoji1787]
Muache wizi mtafika mbali
 
Lakini binafsi naona huwa ni watu wazuri ,

Sizani kama utaona wananchi wakipigwa risasi na askari,

Tarajia kutosikia hayo,

Huwa wanapenda kuona au kusikia haki ikitendeka kwa watu,

Hawapendezwi na dhuruma na kuoneana.

Kama Kweli ni Mzanzibar basi tutarajie utendaji ulotukuka,

Tumuunge mkono na kum-support kwa juhudi ili tufukie malengo.

Tunasubiri Kwa hamu kubwa swala la Katiba Mpya ya JMT ,

Kwenye mambo ya msingi ya kuanza nayo kwenye checklist yako anza na Hilo na Tume huru ya uchaguzi.
Uzuri wa watu hautokani na sehemu, ni hulka tu ya mtu. Huko zenj si ndio kulikua hadi na mazombi wanaotumwa kuua watu

Ooopss maalim huko si ndio kila uchaguzi alisema watu wake wanavuliwa

Anaweza kuwa mzuri sana lakini sio sababu ya uzanzibari wake.
 
Back
Top Bottom