Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Basically sio Demotion ni heavy promotion hiyo
Balozi awe juu ya katibu mkuu kiongozi? Unamaanisha hadi hoyce temu, polepole, togolani n.k wapo juu ya katibu mkuu kiongozi? Balozi boss wake ni katibu mkuu wizara ya mambo ya nje.

Kwa hiyo katibu mkuu wa wizara yupo juu ya katibu mkuu kiongozi? Huendaa hujui katibu mkuu kiongozi ni nani
 
Una uhakika mkuu tiss sio jeshi rasmi
Unajua vyeo vyao kama ni jeshi 🤣🤣🤣🤣 halafu bosi wao anaitwa mkurugenzi,

Kwaio unataka kufananisha TISS na FBI? maana hata CIA ni informants tu japo wana mafunzo ya kila namna, kuna taarifa zitafanyiwa kazi na wanasiasa zingine Jeshi kutegemeana na aina ya taarifa na mlaji wa hio taarifa ni nani
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za viongozi Serikalini Ikulu jijini Dares Salaam, leo tarehe 03 Januari, 2023.

Amesema “Mtakumbuka kuwa Novemba 2022, Bunge la Tanzania lilikuwa na mjadala mzito kidogo kuhusu matumizi ya fedha na madaraka katika ofisi zetu za Kibalozi zilizopo Nchi mbalimbali, Serikali inafanyia kazi kasoro zilizoelezwa ili kurudisha hadhi ya balozi zetu.

“Nimefanya mabadili katika ofisi ya Ubalozi iliyopo New York, ambayo inakuwa na Mwakilishi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.

“Ofisi hii ni muhimu kwa Nchi yetu kwa kuwa ndio inatuwakilisha katika mambo yanayojadiliwa na mataifa na taasisi za kimataifa zilizo chini ya Umoja wa Mataifa Mjini New York.

“Ofisi yetu hiyo inahitaji mwanadiplomasia mahiri anayejua siasa za kimataifa, mzalendo kwa nchi yake na mtulivu wa hekima na busara.

“Hivyo nimeamua kumrudisha nyumbani Prof. Kennedy Gaston aliyeko Ofisi ya New York na kumpeleka Hussein Othman Kattanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

“Kattanga anaenda kuiwakilisha Tanzania kama Balozi wa Kudumu huko New York.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi itajazwa na DKT. Moses Mpogole Kusiluka aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Ikulu itajazwa na Diwani Athuman Msuya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

“Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa itajazwa na Said Hussein Massoro aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za ndani za TISS.”

Mkurugenzi Usalama wa Taifa mpaka Katibu Mkuu ni kupanda au kushuka
 
Ili kuendana na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi 2023,Mh.Rais aendelee kufanya mabadiliko mengine mengi atakayoona inafaa.
Bado tuna safari ndefu 2035 ingawa kwa long plan ni muda mchache sana.
 
Haya mabadiliko yatateremsha bei ya maharage kilo sh. 4500 hali mbaya huku mitaani.
Possibly itawezekana maana mvua zimenyesha sana na wakati huo jamaa zetu Wanasiasa wanaingia mtaani kupoza njaa za chawa wao.
 
Promotion ya kutoka kuwa Karibu Mkuu kiongozi hadi kuwa balozi Marekani na wa kudumu UN?
KM ndio boss wa mabalozi wote
Sio mbaya kujitekenya na kucheka...hiyo ni demotion. Badala ya kuchagua watu, wewe unachaguliwa na kukaguliwa
 
Unajua vyeo vyao kama ni jeshi 🤣🤣🤣🤣 halafu bosi wao anaitwa mkurugenzi,

Kwaio unataka kufananisha TISS na FBI? maana hata CIA ni informants tu japo wana mafunzo ya kila namna, kuna taarifa zitafanyiwa kazi na wanasiasa zingine Jeshi kutegemeana na aina ya taarifa na mlaji wa hio taarifa ni nani

Unajua vyeo vyao kama ni jeshi 🤣🤣🤣🤣 halafu bosi wao anaitwa mkurugenzi,

Kwaio unataka kufananisha TISS na FBI? maana hata CIA ni informants tu japo wana mafunzo ya kila namna, kuna taarifa zitafanyiwa kazi na wanasiasa zingine Jeshi kutegemeana na aina ya taarifa na mlaji wa hio taarifa ni nani
Mkuu Mimi nimekuuliza tiss sio jeshi rasmi Hilo ndo suala langu..
 
Back
Top Bottom