Rais Samia awaleta Global Tree na uwekezaji wa TZS 230BL Tanzania

Rais Samia awaleta Global Tree na uwekezaji wa TZS 230BL Tanzania

Happy Boxing Day kwa hisani ya Mhe Samia Suluhu Hassan
 
Miradi yote iliyoachwa na Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli Rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza kwa 100%

Sihiyo tu tayari mingine mipya inaendelea na Ujenzi,

Tunawajibu wa kumwombea Mama huyu,
 
#2025Fever itawapotezea muda wenu bure,hakuna wakumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi hizi kubwa na nzuri anazozifanya,

#KAZIIENDELEE NA MAMA
 
Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
===
Ajira hizo Watanzania wenzangu, kidogo kidogo tu mtamwelewa na mtaelewa nia njema za mama yetu mnyenyekevu Mhe Samia Suluhu Hassan kwenye safari zake za nje,


Dodoma, Tanzania.

Naibu wa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameongoza jopo la serikali katika Mazungumzo ya awali na kampuni ya Global Tree ambayo inajihusisha na miradi ya kimazingira kwenye kilimo.

Mheshimiwa Bashe amesema “Mazungumzo yetu ya awali yamejikita zaidi kuandaa mradi mkubwa wa kupanda mazao yenye asili ya miti ambayo itamsaidia mkulima kupata kipato na sio tu kuwa na pori ambalo siku ya mwisho mkulima itamchukua muda mrefu kupata mapato ya moja kwa moja.”

Bashe anaendelea kusema kuwa “Mazungumzo haya yanalenga kuanzisha kituo cha pamoja ambapo kupitia taasisi zetu za TARI na ASSA watakuwa na jukumu la kuanzisha Vitalu na miundombinu ya Umwagiliaji kwa ajili ya miche ya Korosho, Kakao, Makademia (Katanga Miti), Michikichi na Kahawa.”

Aidha Bashe alipoulizwa kuhusu muundo wa utekelezaji wa mradi alisema “Mradi huu utakua wa ushirikiano wa pamoja baina ya serikali na sekta binafsi (PPP) na miti hii itakua ni ile ambayo tunazalisha wenyewe Kwa njia za asili pamoja na njia za kisasa za urutubishahi.”

Kuhusu gharama za mradi Bashe alisema “Mpango wa uwekezaji wa mradi huu una thamani ya dola za kimarekani Milioni mia moja sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni mia mbili thelathini.”

Aidha, uwekezaji huu utajikita katika kumuwezesha mkulima bila kuwa na mzigo wa kulipia gharama za awali za uwekezaji kwakua Mradi huu mbali na kuwa na tija kwenye kilimo pia utakuwa mradi wenye toja kubwa kwenye mazingira huku lengo la msingi likuwa ni kuboresha maisha ya watanzania wengi wanaotegemea kilimo kama sehemu ya msingi ya kipato cha kuendeshea familia.

Naibu Waziri Bashe aliongeza ya kuwa “Hata hivyo bado tunachangamoto nyingi kwenye sekta ya kilimo ingawa mabadiliko na muelekeo wetu wa kisera juu ya kuruhusu uwekezaji binafsi kwenye sekta hii Kwa sehemu kubwa utatatua changamoto hizi hasa za mitaji kwa wakulima wadogo na kuongeza tija ya Kilimo.”

View attachment 2045762

View attachment 2045763

View attachment 2045764
Kazi ifanyike zaidi na zaidi,
 
Back
Top Bottom