Pre GE2025 Rais Samia awalipua watu kwa shangwe, nderemo na vifijo mitaani baada ya kuwahakikishia kuwepo Madarakani hadi 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Mitaani ni shangwe, nderemo, vifijo , chereko chereko,furaha,hoihoi na tabasamu tupu kwa wananchi mbalimbali. Hii ni baada ya Rais Samia kukata kiu ya mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo mioyoni mwao. Kiu ya kutaka kuona Rais Samia akiendelea na muhula wa pili wa Urais kwa kuchukua ,kujaza na kurejesha Fomu ya Urais.

Shangwe hiyo imekuja baada ya Rais Samia kutamka hadharani kuwa anataka kuacha alama katika uongozi wake atakapokuwa anajiandaa kurejea Nyumbani Kizimkazi na kuja kuwahoji walipofikia kimafanikio na kimaendeleo katika Masuala Mazima ya ushirika na ugani.

Kauli ya kusema kuwa atakapo Kuwa anajiandaa kurejea Kizimkazi miaka hiyo ya mwishoni kuelekea 2030.imemaanisha kuwa Rais wetu Mpendwa amekubali Ombi na Maombi ya Mamilioni ya watanzania wa makundi mbalimbali waliohitaji kuona akiendelea kuwa Rais Wetu.

Ndio maana makundi kama Walimu walikuwa wamemchangia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuchukulia Fomu ya Urais.pia wahandisi nao pia walikuwa wamechanga mamilioni ya pesa kwa ajili ya kumpatia Usafiri wa helikopta atakayo kuwa anaruka nayo angani na kuteka anga lote la Tanzania kikomandoo wakati wa kampeni,huku bendera ya kijani ikipepea angani.

Kwa hakika Rais Samia ameleta furaha kubwa sana hapa Nchini kwa kauli yake hiyo.ikumbukwe ya kuwa mamilioni ya watanzania chaguo lao ni Rais Samia tuu hapo Mwakani. Watu wengi sana walikuwa wamesema kuwa wanahitaji kuona CCM ikimpatia Rais Samia ugombea Urais.jambo ambalo hata hivyo CCM kupitia viongozi wake ilijibu kwa kusema kuwa Ni Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.

Kwa hakika Rais Samia ndiye ameshikilia Furaha ya Mamilioni ya watanzania.kama Ingetokea akakataa ombi la watanzania,kwa hakika angewakatisha sana tamaa na kuwavunja moyo mamilioni ya watanzania ambao kwa sasa wamejaa matumaini tele na uhakika wa kutimiza ndoto zao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kweli anatosha Hadi nimetokwa na machozi !ndio maana hao walimu waligoma huko Mbeya !!
 
🤣🤣 mitaa gani hiyo ila machawa 🤣🤣🤣🤣 🚮🚮
 
Eti "Kuripua" acha kuharibu lugha wewe chawa ni " Kulipua".

Halafu labda ailipue nchi kwa ufisadi uliotamalaki huku yeye akiwa anajiita ni chura kiziwi.

Mafisadi na majizi yaliyotajwa kwenye ripoti ya CAG yanapeta huko mitaani na hakuna hatua yoyote wamechukuliwa.

Kagawa bandari na mbuga zetu kwa waarabu huko ndio kulipua nchi kwa shangwe chawa?
View attachment 3066251
Ripoti ya CAG kila siku itakuwa kichekesho;
"Rushwa katika Mahakama,
Bila kusahau ufisadi wa Polisi,
Halafu hao TISS ndiyo wenyewe
Halafu wanajeshi wamesahau kulipa bili ya Tanesco"

Kwa mpango wa namna hii,nani atamkamata nani?
 
Kwa kwli nimesoma bandiko lako huju nikiwa nabubujikwa na machozi kwa huzuni
 
2015 na 2020 Ni Mama Yako ndio alikuwa anapiga kampeni na picha na jina lake vilikiwa kwenye mbao za wagombea?
Wewe mpuuzi hata kusoma kumbe hujui achilia mbali kuelewa ?

Nimeuliza swali jepesi sana lini Samia aliwahi kuwa "presidential aspirant" wa CCM , au huelewi lugha ? , nilimaanisha ni lini Samia aliwahi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM jibu ni kuwa Samia hajawahi kugombea urais na kwa sasa huyu ni rais wa mpito baada ya kufariki mtangulizi wake hivyo Samia atakuwa mgombea 2025 kama akifanikiwa kuwepo au kama CCM wakimpitisha.

Hivi kumbe ili uwe chawa kigezo cha kwanza ni lazima uwe zezeta, basi nimethibitisha hilo.
2025-30 Rais ni Samia imeisha hiyo na atashinda Kwa kishindo ,mapovu mtaishia kumwaga jf tuu.
Kishindo kipi??

Kwa huu upuuzi mnaondesha Tanzania ndio unaita uchaguzi??

Hata wapinzani wakishiriki tena huu upuuzi 2025 nitawashangaa maana kipi kimebadilika tangu ule ushenzi uliofanyika 2020?

CHADEMA wakishiriki uchaguzi huo bila tume huru basi wasije kusema wameibiwa maana wanajua nyani ni wale wale ila pori tu ndio tofauti, kipindi kile mwizi alikuwa mwanaume ila kipindi hiki ni mwanamke.
 
Wewe mpuuzi hata kusoma kumbe hujui achilia mbali kuelewa ?

Nimeuliza swali jepesi sana lini Samia aliwahi kuwa "presidential aspirant" wa CCM , au huelewi lugha ? , nilimaanisha ni lini Samia aliwahi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM jibu ni kuwa Samia hajawahi kugombea urais na kwa sasa huyu ni rais wa mpito baada ya kufariki mtangulizi wake hivyo Samia atakuwa mgombea 2025 kama akifanikiwa kuwepo au kama CCM wakimpitisha.

Hivi kumbe ili uwe chawa kigezo cha kwanza ni lazima uwe zezeta, basi nimethibitisha hilo.

Kishindo kipi??

Kwa huu upuuzi mnaondesha Tanzania ndio unaita uchaguzi??

Hata wapinzani wakishiriki tena huu upuuzi 2025 nitawashangaa maana kipi kimebadilika tangu ule ushenzi uliofanyika 2020?

CHADEMA wakishiriki uchaguzi huo bila tume huru basi wasije kusema wameibiwa maana wanajua nyani ni wale wale ila pori tu ndio tofauti, kipindi kile mwizi alikuwa mwanaume ila kipindi hiki ni mwanamke.
Mama yupo Hadi 2030,povu halitakusaidia na huna Cha kufanya 😁😁😁😁
 
Mama yupo Hadi 2030
Hata machawa wa Magufuli walisema, Magufuli atakuwepo hadi 2025 je yupo wapi?
,povu halitakusaidia na huna Cha kufanya 😁😁😁😁
Huyo ni mama yake Abdul sio mama yako.

Hakuna mahali kwenye katiba hii hii mbovu pameandikwa mgombea atagombea nafasi ya "Mama" huyo aitwe rais na akosolewe kwa kupwaya kwenye nafasi ya urais sio kumuita kwa lugha laini laini huku anaonyesha madhaifu ya kiuongozi.
 
Na atakaye kubishia unaweza kumgonga na ile pukipiki ulioyopewa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mitaani ni shangwe, nderemo, vifijo , chereko chereko,furaha,hoihoi na tabasamu tupu kwa wananchi mbalimbali. Hii ni baada ya Rais Samia kukata kiu ya mamilioni ya watanzania waliyokuwa nayo mioyoni mwao. Kiu ya kutaka kuona Rais Samia akiendelea na muhula wa pili wa Urais kwa kuchukua ,kujaza na kurejesha Fomu ya Urais.

Shangwe hiyo imekuja baada ya Rais Samia kutamka hadharani kuwa anataka kuacha alama katika uongozi wake atakapokuwa anajiandaa kurejea Nyumbani Kizimkazi na kuja kuwahoji walipofikia kimafanikio na kimaendeleo katika Masuala Mazima ya ushirika na ugani.

Kauli ya kusema kuwa atakapo Kuwa anajiandaa kurejea Kizimkazi miaka hiyo ya mwishoni kuelekea 2030.imemaanisha kuwa Rais wetu Mpendwa amekubali Ombi na Maombi ya Mamilioni ya watanzania wa makundi mbalimbali waliohitaji kuona akiendelea kuwa Rais Wetu.

Ndio maana makundi kama Walimu walikuwa wamemchangia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuchukulia Fomu ya Urais.pia wahandisi nao pia walikuwa wamechanga mamilioni ya pesa kwa ajili ya kumpatia Usafiri wa helikopta atakayo kuwa anaruka nayo angani na kuteka anga lote la Tanzania kikomandoo wakati wa kampeni,huku bendera ya kijani ikipepea angani.

Kwa hakika Rais Samia ameleta furaha kubwa sana hapa Nchini kwa kauli yake hiyo.ikumbukwe ya kuwa mamilioni ya watanzania chaguo lao ni Rais Samia tuu hapo Mwakani. Watu wengi sana walikuwa wamesema kuwa wanahitaji kuona CCM ikimpatia Rais Samia ugombea Urais.jambo ambalo hata hivyo CCM kupitia viongozi wake ilijibu kwa kusema kuwa Ni Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.

Kwa hakika Rais Samia ndiye ameshikilia Furaha ya Mamilioni ya watanzania.kama Ingetokea akakataa ombi la watanzania,kwa hakika angewakatisha sana tamaa na kuwavunja moyo mamilioni ya watanzania ambao kwa sasa wamejaa matumaini tele na uhakika wa kutimiza ndoto zao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mwambie aje Ukumbi wa Mwalim Nyerere apate Daawa, We an international speakers from all over the world including UK .. Its so lovely to be in Dar re salaam today.
 
Hata machawa wa Magufuli walisema, Magufuli atakuwepo hadi 2025 je yupo wapi?

Huyo ni mama yake Abdul sio mama yako.

Hakuna mahali kwenye katiba hii hii mbovu pameandikwa mgombea atagombea nafasi ya "Mama" huyo aitwe rais na akosolewe kwa kupwaya kwenye nafasi ya urais sio kumuita kwa lugha laini laini huku anaonyesha madhaifu ya kiuongozi.
Kwani una Mpango wa kumfanya nini my.Rais?
 
Nasikitika kwamba Rais Samia anataka kukaa madarakani mpaka 2030.

Siku moja walifika wageni hapa, watoto wa shule, nilikuwa naongea nao,nasema," Sikilizeni nyinyi watoto,kama watu wanazeeka,it is because of their careless lifestyle. If you live sensibly,you can remain alive for an incredibly long period of time."
Nilipozungumza maneno hayo nilileta taharuki kubwa sana hapa nyumbani.
Vijana wanawaza,"Huyu jamaa vipi tena? Tunamsubiri afe tuifaidi hii nyumba yeye anataka kuishi milele tena?"
 
Back
Top Bottom