Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
 
Kwa kweli tukisema muacheni Mh Hayati Magufuli apumzike mahali aliko tunashambuliwa eti sisi ni sukuma geg! Jaman marehemu kwa heshima za Afrika huwa tunamwacha apumzike aliko kuliko kumsemea vibaya vibaya.

Leo nimesikia Mh Raisi akisema utawala wa awamu ya Tano ulitengeneza nidhamu ya uwoga kwa watumishi, kwa sababu ulikuwa ni Simba, alikuwa ukizingua anakungata ngwadu!

Sasa kwa Nini ustekeleze unavyotaka. Paspo kumsem mwenda zake?
 
Leo Ni zamu ya Nani kulinda kaburi Chatto?
 
Back
Top Bottom