Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Hao ndio wana CCM wakiwa katika ubora wao wa unafiki. Hapa juzi kati tu, yaani tarehe 17-03-2022 siku ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha JPM, walienda Chato na kuahidi kumuenzi shujaa wao.

Huku wakiwa wamevaa nguo nyeusi kama alama ya maombolezo, zilitolewa hotuba zenye maneno mazuri na yenye kuleta hisia juu yake, na ungewaangalia sura walionyesha kana kwamba bado wana huzuni nzito mioyoni meao, na wengine hata walijipigapiga vifuani pale walipoliona kaburi lake. Lakini leo hata mwezi haujapita wanaanza kumtolea maneno mazito yenye kuukosoa utawala wake.

Kumbe ndiyo sababu hotuba fupi ya mjane wa marehemu, mama Janeth iliweza ku "steal show" siku hiyo. Ilidhihirisha wazi ya kuwa chama hakikufanya maandaluzi yoyote juu ya siku hii, na hata mualiko wa kwenda Chato ilikuwa ni jitihada binafsi za mama Janeth mwenyewe, na ilikuwa ndiye hasa aliyemualika Mwenyekiti Taifa!
 
Huyu mama anataka uwachekee watumishi wa umma.

Heshima ya moyoni hiyo haipewe serikalini, hiyo inatolewa nyumbani.

Huyu mama ni kimeo.
Dah....huyu ni kimeo kwa kweli.....Wala haya siyo yakutamkwa na yeye....VP kwa zaidi miaka 5.....
Asichokijua ....HOFU....WOGA...ndiyo mwongozo mkuu wa maisha ya binadamu.....bila ya vitu hivi hakuna maisha......
Hata HESHIMA nayo hujengwa na HOFU na WOGA.......
Wanafunzi husoma kwa bidii kwa HOFU ya kushindwa mitihani yao..... Waumini huogopa kutenda dhambi kwa sababu ya HOFU ya kwenda motoni......ili watumishi wa umma wawajibike lazima wawe na HOFU ya kupoteza ajira/mishahara.......atashangaa pia akijua wengi wanamuheshimu kwa sababu ya HOFU ya kwenda jela....au Basi 🤭
 
Huyu dada afanye yake aache kuzungumza mambo ambayo yamemshinda kwa hizi kauli naona ni kampeni tu hana lolote,hawezi kuwasimamia watanzania Sasa anatafuta njia yake ili wampende haha! Sijui kwanini anatafutwa kupendwa kwa kumponda mwengine tena mfu!.. watanzania msipokuwa na vichwa vizuri Hawa wanasiasa watatuendesha kama gari bovu!
 
Umemuelewa lakini?. Kasema watu wawe na nidhamu ya moyoni sio ya kinafiki. Maana nidhamu ya kinafiki ni ya muda na Wala haisaidii.
Bila Shaka Sasa watu wana nidhamu ya moyoni
 
mama samia hukupaswa kumsema hadharani kuonyesha chuki zake kwa jpm sababu walikuwa pamoja wanapanga mipango pamoja na unashauriana, haikuwa vizuri kusema mama ni dhaifu na ana roho mbaya, afadhali angekuwa hakuwa katika madaraka pamoja na jpm yeye kachaguliwa hapo sawa.angalia kenya makamo wa rais ruto anamkatalia kenyatta na kumpinga mbele ya wananchi. mama ulishindwa nini kujiudhuru. mbona ulikuwa ukimsifia hadharani
 
mbona jiwe na yeye alikuwa anawananga watangulizi wake hasa Jk

Acha mzani ubalance

alikuwa anamnanga jk akiwa kikwete yupo hai sio kafa na jpm hakuwa naibu rais wa kikwete alikuwa yupo chini waziri tu hana sauti kwa rais lakini mama yeye alikuwa naibu rais mpo pamoja kosa la jpm ni kosa la naibu pia. mkisifia mazuri aliyoyafanya makufuli mnamsifia na mama walikuwa pamoja. akisemwa ubaya wake jpm anasemwa kama yeye, mbona hakuna mradi wowote ulioanzishwa na mama yote bado ni ya jpm
 
Lakini maza kuna mambo angeyanyamazia tu.
Hili litamharibia sana.
Watanzania wana utoto mwingi...hili litawaharibu sana watumishi wa umma na watajiachia mno kwa kauli hii
Hebu mtumishi wa umma ajiachie aone moto!!
Rais hajasema wasiwe na nidhamu, amekazia wawe na nidhamu tena ile ya moyoni ndio chanya zaidi.Nidhamu ya woga mbaya naweza kufanya kwa savabu uko mbele yangu, ukinipa kisogo napuyanga.
Mama yetu mhe Rais kazi iendelee.
 
Kwa ujumbe yupo sawa ila hapo kwenye Simba wa Yuda hajaenda sawa Simba wa Yuda haina maana ya mtu katili. Halafu kwa wakristo amefanya dhihaka sana tu anamlinganishaje Yesu na vitu ajabu namna hii. Mama awe anatafakari Maneno ya kuongea kabla, yeye ni raisi ujue.
 
Watanzania tuache UONGO
Hakuna Utawala uliokuwa na hofu km wa Magufuli hata katika chart Duniani tuliongoza au tulikuwa karibia na mwisho kwa wasiokuwa na furaha
Mama aliona na kusikia mwenyewe viroba vya maiti ufukweni, watu wakipotezwa wakati wameingia mlangoni, Mara ngapi aliachia ngazi na kurejeshwa kwa nguvu, wake za viongozi waliomtangulia jakuwanyanyasa kwa vitisho mpaka akakemewa na viongozi wake wa Dini na kuja kutoa ubunge?
Ukitawala kwa kurarua (upanga) mawe utararuliwa
Sio maofisini tu hata mitaani alipaharibu, mtu unatokea shift usiku huruhusiwi kuingia papote upate kilagi mpaka saa 10 jioni jumamosi usifungue Duka TRA wanakudai, account Benki zinaporwa ACHENI AKAPUMZIKE
 
Ila wanasiasa kweli wana mioyo ya ajabu sana. Inamaana mother alisimamia asiyoyaamini. Asa kwa nini tangu siku ya kutangaza kifo chake alimpa sifa kibao hadi juzi kwenye matanga ya mwaka mmoja alizidi jumla sifa? Yaan hawa watu hawaaminiki akikwambia habar za asubuhi, kabla ya kuitikia angalia muda Kwanza inaeza kuwa jion na wewe ukaungana nae kuifanya iwe asubuhi.
 
Wacha mama atufumbue macho maana jiwe alikuwa ameamua kutufanya vipofu.
 
Mkuu hilo la kumlinganisha jiwe na yesu lilianzia kwa Lugola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…