mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Hao ndio wana CCM wakiwa katika ubora wao wa unafiki. Hapa juzi kati tu, yaani tarehe 17-03-2022 siku ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha JPM, walienda Chato na kuahidi kumuenzi shujaa wao.
"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.
“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.
“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma
---
Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.
Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.
Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Huku wakiwa wamevaa nguo nyeusi kama alama ya maombolezo, zilitolewa hotuba zenye maneno mazuri na yenye kuleta hisia juu yake, na ungewaangalia sura walionyesha kana kwamba bado wana huzuni nzito mioyoni meao, na wengine hata walijipigapiga vifuani pale walipoliona kaburi lake. Lakini leo hata mwezi haujapita wanaanza kumtolea maneno mazito yenye kuukosoa utawala wake.
Kumbe ndiyo sababu hotuba fupi ya mjane wa marehemu, mama Janeth iliweza ku "steal show" siku hiyo. Ilidhihirisha wazi ya kuwa chama hakikufanya maandaluzi yoyote juu ya siku hii, na hata mualiko wa kwenda Chato ilikuwa ni jitihada binafsi za mama Janeth mwenyewe, na ilikuwa ndiye hasa aliyemualika Mwenyekiti Taifa!