Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Huyu mama anataka uwachekee watumishi wa umma.

Heshima ya moyoni hiyo haipewe serikalini, hiyo inatolewa nyumbani.

Huyu mama anaishi kwenye nadharia ya wapi sijui.

Hofu ndio msingi wa kila kitu, mwanafunzi bila hofu ya kushindwa mtihani hawezi kusoma, binadamu bila hofu ya mungu atatenda dhambi (kama wanavyodai waumini wa dini)

Mfanyakazi wa Serikali asipokua na hofu ya kupoteza kazi na mshahara sasa hapo huyo ni mfanyakazi ama ndie muajiri?

Mtoto lazima awe na hofu kua nikifanya kosa hili baba ataniadhibu,

Hofu ndio inaongoza Dunia, hofu ya kutenda jambo kinyume na kuadhibiwa ndio inasabaabisha watu wanaogopa kutenda mambo mabaya kwa hofu ya kuadhibiwa.

Huyu mama mwambieni hawezi kuongoza nchi kwa hisia. Wanaomdanganya matokeo yake atauaona sio muda mrefu.

Tujiulize, enzi za mentor wa huyo mama, Kikwete, wafanyakazi wa serikali hawakua na hofu na chochote, asipokuhudumia mwananchi hana hofu yoyote ya kupoteza kazi, hana hofu ya kuiba mali za umma, hana hofu ya kuwahi kazini nk, na wakati wa awamu ya 5 ambako wafanyakazi wa serikali walijengenwa hofu ni wapi kulikua na faida kwa wananchi?

Huyu mama ni kimeo.
 
Huyu ni ndumilakuwili,mbona aku step down

Tuseme tu ukweli umejaribu kwenda kwenye taasisi za serikali ukaona huduma zao zikoje ukifananisha na simba wa chato huduma ilikuaje.
Watu walikuwa wanaishi kwenye maisha ya uoga tu hakuna cha unafuu.

Magufuli alikuwa anatishia watu tu na wakati mwingine aliwafanyia ubaya vilevile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…