Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Muheshimiwa,kufukuzwa kazi ni sehemu ndogo sana katika utumishi iwezayo kumtokea mfanyakazi.Hatupaswi kuwajenga watumishi kwa fikra za kufukuzwafukuzwa.Bali,wajengewe matumaini ya kudumu,kustawi na kuufurahia utumishi.Kufukuzwa iwe ni kama ajali tu.
Acha kujitoa akili, Africa hakunakitu kama hicho ndio maana kurazinaibiwa mchana kweupe, huo usmati wa moyoni unaanzia wapi.
 
Acha kujitoa akili, Africa hakunakitu kama hicho ndio maana kurazinaibiwa mchana kweupe, huo usmati wa moyoni unaanzia wapi.
Kuna mambo unachanganya.Wanasiasa,watumwa na watumishi.Mtumishi ni mtu unayetegemea akupe tija.Siyo mtumwa wako yule.Unapaswa kuenda naye kwa hekima,busara na akili.Unapo-refer Afrika,huko ni kujidharau kwako na kuonesha kwamba haupendi na hautaki kutoka kwenye boksi.Mentalities za kutawaliwa na mzungu.Mjenge mfanyakazi akupe tija.Siyo kumtisha.Mara ntakufukuza,mara ntakutumbua.Ni ujinga ambao hauleti tija.
 
Kwa kweli tukisema muacheni Mh Hayati Magufuli apumzike mahali aliko tunashambuliwa eti sisi ni sukuma geg! Jaman marehemu kwa heshima za Afrika huwa tunamwacha apumzike aliko kuliko kumsemea vibaya vibaya.

Leo nimesikia Mh Raisi akisema utawala wa awamu ya Tano ulitengeneza nidhamu ya uwoga kwa watumishi, kwa sababu ulikuwa ni Simba, alikuwa ukizingua anakungata ngwadu!

Sasa kwa Nini ustekeleze unavyotaka. Paspo kumsem mwenda zake?
Ndugu,

1. Waliokufa huwa wamekufa na kuzikwa chini ya ardhi na kugeuka udongo/mavumbi.

Hawaendi huko kupumzika !!

2. Kinachojadiliwa hapa ni matokeo au alama (footprints) alizoziacha mtu aliyekwisha kufa. Kwa hapa ni kesi ya Magufuli

Kwa hiyo hata ulie na kumwaga ndoo nzima ya machozi ili Magufuli aachwe kwa kile unachoita "kupumzika", hiyo haiwezi kufuta footprints zake mbaya au nzuri

KUKUSAIDIA WEWE, FANYA HIVI;

✓Ukiona mtu wako aliyekwisha kufa anasemwa kwa mabaya, na ikakuuma; basi wewe mseme kwa mazuri yake.

✓Mizani ikiegemea upande wa mazuri, utashinda na utakuwa na furaha.

✓Lakini ukishindwa kuii namisha mizani upande wako, basi jua kuwa umeshindwa wewe na mtu wako.

✓ All you have to do is to accept and take responsibilities!!
 
Kasema ukweli,ila tangu ameingia yeye mbona huduma zinazidi kudidimia? Nijuavyo mm Mtanzania hutakiwi kumchekea ktk kazi, kwasababu wengi tunatafuta kazi ila tukipata kazi hatupendi kufanya kazi,nchi yetu Ina watu wa ajabu sana......... inawezekana JPM alichokuwa anafanya alikuwa anakosea ila bila vile Mtanzania ninayemjua mm na ningumu kuwa effectively and efficiently eneo la kazi,tunaongoza Kwa visingizio.

Bila ukali Kwa public servants......hutoboi
 
Kwani watu hawawezi kufanya kazi bila kumtaja Ngosha!
😀😀 wanaamini wakimtajataja ndio wataonekana wanafanya kazi.

Magu amefanya kazikubwa sana ya kutukuka sasa kila wakifurukuta kujaribu kumfikia wanaona pagumu ndio maana wanaamua kufanya kazi ya kupaka matope iliwatu wamchukie kituambacho milele hakitawezekana hapa Tz.

Naona anamjiausiku kama alivyo semamwenyewe.
 
Mama alete na faili la SHUJAA la Mirembe tujadili 😂😂
 
View attachment 2172780

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.

So inategemea kumfundisha Babu kinana kubweka. Nyie watanzania mna ugonjwa gani. Nidhamu haijengwi chuoni. Ni nyumbani na shuleni kwa pamoja.
 
Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.
...No comment
 
Back
Top Bottom