Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

S
Sometimes tunapaswa kuwa wakweli.
Wakati wa Simba wa Yuda:-
(1) Umeme haujawahi kukatikakatika kihuni kihuni kama ilivyo sasa.
(2) Mfuko wa mbolea ulinunuliwa kwa sh. 50,000/- lakini sasa ni sh.120,000/-
(3) Hakukuwa na Ajali nyingi za magari kama ilivyo sasa.
(4) Hakukuwa na visa vingi vya mauaji kama ilivyokuwa miezi michache iliyopita.
(5)Watu wakienda kwenye ofisi za umma walihudumiwa haraka bila ubabaishaji tofauti na inavyoelekea sasa.
(6)Niliwahi kuishi MAKAMBAKO miaka ya 2012/2015, wakati ule ilikuwa ukitembea mitaani kuanzia saa 2 za usiku unapigwa NONDO kichwani, lakini alipoingia Simba wa Yuda NONDO zote zilitoweka ghafla.
Kama mimi ni mwongo, nenda ukawaulize watu wa MAKAMBAKO.
(7) Bei za vitu hazijawahi kupanda kama ilivyo sasa.
Hayo ni machache tu.
Mpaka hapo, utaachaje kumpenda SIMBA WA YUDA?
Utaachaje kumkumbuka SIMBA WA YUDA?
RIP, SIMBA WA YUDA.
Sisi hatutakusahau kamwe hata kama watatengeneza mbinu mbalimbali za kutufanya tukusahau.
RIP, DAD.

Vyote ulivyosema sio ukweli. Kwani sukari imepanda kipindi Cha Nani?.

Halafu kuhusu ajali mbona zilikiwepo nyingi?. Umesahau ajali ya meli ya ukerewe, ajali ya city boys , ajali ya morogoro waliokufa watu 100.

Kwangu Mimi Magufuli alikuwa mpenda sifa na Wala hakufanya Mambo kwa upendo .
 
Jiwe aliitawala nchi kwa mikwara mingi
Ambacho hulioni ni kuwa na Mh. SSH ni mikwara tuu. Tatizo lipo kwenye Hamaki. zina Ulegevu na Dhihaki na kubeza.
Wote himaya moja.
Yule Simba alikuwa hana hata na Hamaki za kudumaza, kubeza na kudhihaki....lakini pale utaapo amini kuwa kulikuwa hakuna "majizi" wezi na wahujumu nchi, basi kweli yake yalikuwa Mikwara. . Food for thought...Simba huwa sio mikwara tu, "Huraruararua".
 
Katika kipindi cha awamu ya tano kulikuwa na remarkable changes kwenye utoaji huduma ktk civil service offices.

Generally speaking Rushwa ilipungua, na speed na ubora wa utoaji huduma viliongezeka. Kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu, ile dhana ya cheo ni dhamana ilihuishwa, na ilionekana in action. Watumishi waliamka.

Mabadiliko hayo yaligusa maisha ya kila siku ya watu wengi wa hali ya chini. And thats what mattered to majority. Ndio maana walijitokeza kwanwingi kumzika Magufuli, then man behind hayo mabadiliko ya kiutendaji.

They dont give a sh!t whether nidhamu iliyoonekana kipindi hicho ilitoka Moyoni, Matvkon! au puani. What matters ni kwamba ilikuwepo. And for once baada ya muda mrefu Utu wao na Haki zao viliheshimiwa.
 
Mama atafute washauri wazuri,shida anakumbatia washauri ambao nao nchi iliwashinda kuongoza "Msoga gang".
 
Unachopanda utavuna! Yeye alimchafua rais aliyemuachia madaraka ni zamu yake kuchafuliwa! Ben saa nane! Tundu lissu! Azory gwanda! Na wengine wengi ni wahanga wa utawala wa jiwee!
 
I
Umemuelewa lakini?. Kasema watu wawe na nidhamu ya moyoni sio ya kinafiki. Maana nidhamu ya kinafiki ni ya muda na Wala haisaidii.
Na hyo nidhamu ya kinafiki mbona ipo sana hapa Bongo,kuanzia huko serikalini watu wakoradhi kukipigia makofi hata kama umekosea hakuna wakuinua mdomo kusema wataishia kusema pembeni, wakilinda matumbo yao
 
Kuna mambo unachanganya.Wanasiasa,watumwa na watumishi.Mtumishi ni mtu unayetegemea akupe tija.Siyo mtumwa wako yule.Unapaswa kuenda naye kwa hekima,busara na akili.Unapo-refer Afrika,huko ni kujidharau kwako na kuonesha kwamba haupendi na hautaki kutoka kwenye boksi.Mentalities za kutawaliwa na mzungu.Mjenge mfanyakazi akupe tija.Siyo kumtisha.Mara ntakufukuza,mara ntakutumbua.Ni ujinga ambao hauleti tija.
Mfanyakazi ukimtishia tishia lazima aanze kufanya hujuma.... kitu ambacho ni hatari mno kwa mfumo mzima wa shughuli yako. Na kama ni msomi ndo hatari inakuwa kubwa zaidi. Ila ukimpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake huwa matokeo yanayoonekana kwa haraka. Kumtishia mfanyakazi ni upumbavu. Mwendakuzimu alizingua mno.
 

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Asante sana mama samia yule mwendazake alikua ibilisi aendelee kuoza milele amen
 
Hakuna anyemkumbuka kwa mema.

Wewe ni mpuuzi sana mkuu. Magufuli alikuwa ni Anti-elite. Kwa tafsiri nyingine, unaweza kusema alikuwa populist. Huwezi kumkuta hata mara moja Magufuli anazungumziwa vizuri kwenye corridors of power, kwasababu agenda yake haikuwa aligned na agenda ya Elites Interests/ The Establishment. Magufuli hakupendwa na Elites, alipendwa na mamilioni ya Watanzania walioomboleza kifo chake na kujitokeza mwa mamilioni kuaga mwili wake na kumzika. Ni mpumbavu peke yake ambaye anaweza ku deny the fact kwamba Common people hawakumpenda Magufuli...
 
Kwa kweli tukisema muacheni Mh Hayati Magufuli apumzike mahali aliko tunashambuliwa eti sisi ni sukuma geg! Jaman marehemu kwa heshima za Afrika huwa tunamwacha apumzike aliko kuliko kumsemea vibaya vibaya.

Leo nimesikia Mh Raisi akisema utawala wa awamu ya Tano ulitengeneza nidhamu ya uwoga kwa watumishi, kwa sababu ulikuwa ni Simba, alikuwa ukizingua anakungata ngwadu!

Sasa kwa Nini ustekeleze unavyotaka. Paspo kumsem mwenda zake?
Aliko anashangaa maana anaona hatumsemi vizuri ,saizi anaungua Kinyama akirudi anafaa kuchemshia ziwa victoria msimu wa baridi
 
Hiyo Simba wa yuda ingetolewa kwenda mashariki Takhbirrrr ingemhusu mtoaji
 
Jiwe aliitawala nchi kwa mikwara mingi
Ndio nakwambia kama ulikuwa hauna amani ya moyo basi ulikuwa unajitesa mwenyewe tu mkuu, maana watu walikuwa wanafurahia maisha kama kawaida sasa huko kukosa amani ya moyo labda ni tatizo binafsi n si kwamba watanzania waliacha kula bata na kufanya mambo yao kwa kukosa amani ya moyo et kisa ni mikwara ya simba wa yuda.
 
Hakuna anaye mpenda
Kwa hoja zipi? Mie nimetoa mfano wa maziko yake hata mie sikutegemea kuwepo ummati ule yani watu waache kazi zao na kwenda kusimama barabarani na viwanjani halafu useme wale wanamchukia kama wewe mkuu?we mbona hukwenda?

Elewa kwamba sio kila mtu alikuwa anaugua kwa kumchukia Jiwe kama mlivyo wengine kiasi hadi cha kujikosesha amani ya moyo.
 
🤣🤣🤣🤣 So mzeya isingekuwa kuna moto ingekuwa full burudani
Unajua kabisa vitu vingi vya dhambi dhambi ndio vitamu sasa kama kusingekuwa na adhabu yeyote kwamba hata ukifanya hayo madhambi hakuna kuadhibiwa kwamba hakuna moto wala nini unadhani watu wangeogopa kufanya dhambi? Dunia tamu.
 
Unachopanda utavuna! Yeye alimchafua rais aliyemuachia madaraka ni zamu yake kuchafuliwa! Ben saa nane! Tundu lissu! Azory gwanda! Na wengine wengi ni wahanga wa utawala wa jiwee!
Wahanga wako wengi hata wauza ngada walijikuta ni wahanga wa utawala wa Jiwe. Wengi walifulia na wengine kuswekwa jela hakika walipitia kipindi kigumu sana.
 
Back
Top Bottom