Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Alikuwa anajua kila kitu, alichokisema pale alikuwa anahadaa umma tu. Hakuna watekaji wowote zaidi ya lile kundi lake la watu wasiojulikana. Katafute walioko usingizini boss.
Kujiandikia tu mambo bila kuwa na evidence nalo ni tatizo.Lete ushahidi na sio porojo.
 
Hapo amefeli kwa kiwango cha kimataifa.
Bila kuwa na hofu nini kitafanyika chini ya jua?
Bila kuwa na hofu, watu watafanya mambo ya ovyo mchana kweupe na kusababisha maumivu kwa watu wengine.
Nenda Korea, Nenda CHINA, Japan nk. Watu wanafanya kazi kwa hofu ndo maana wapiga hatua za maendeleo.
Siku hizi watu hawana hofu, ndo maana wanapandisha bei za vitu kwa kadri wanavyotaka wao.
Angekuwepo JPM upuuzi wa kupandisha bei za vitu kila siku ungekuwepo? La, hasha. Nani angethubutu. Sasa tupo kwenye gari lililo katika mwendo na Dereva ameachia usukani ameshikamana na WAHUNI. Mungu tusaidie.
 
Kama ndio hivyo basi sina mashaka kwamba hata huo mfumo wenyewe hujui ni nini,achilia mbali kujua unajengwa vp!!

Kuna maajabu gani ya kujenga mfumo imara? Au unadhani mfumo ni kitu complex kwa kiwango hicho? Au kwakuwa kwako unaona mfumo ni kitu so percluliar basi unadhani kuna ugumu huo.
 
Rais Samia ulimfukuza kazi mkuu wa mhimili ungine(Bunge) Mzee Ndugai kwa kusema ukweli kama unakopa sana,Je pale hukuwajengea watumishi nidhamu ya uoga kama wakuogope?
Nasubiri jibu toka kwa ‘Chawa’
 
Hizo kauli za karaha hata Magufuli alitumia kwa viongozi wenzake waliomtangulia, au wakati akitumia kauli zile ulikuwa bado hujaanza kufuatilia haya mambo? Ndugu ni hivi, muosha huoshwa.
Utakuwa mjinga mkuu kuamini kosa la mtangulizi litafanya lako kuwa halali.
 
Kuna wakati unaweza kudhania uko sahihi lakini ukawa umekosea sana, si kila neno unaloweza kulitamka ulitamke. Kwenye executive kuna confidentiality and respect to the former executives and their methods.
Unaanzaje kum respect kichaa kama ********? Let's be serious guys Mwendazake alikuwa anaharibu umoja na ustawi wa Taifa letu. He doesn't deserve any respect
 

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Yeye mwenyewe alikuwa havai barakoa, baada ya Magu kuondoka anavaa Barakoa!!
Sasa yeye aseme atafanyaje kuendeleza hiyo heshima bila woga?
Haoni kuwa dawa kwa sehemu kubwa ni kupunguza madaraka ya Rais? Yeye alipo hapo anapewa heshima ya woga!!
 
Serekali yote sasa hivi iko mitandaoni, maamuzi yake yanategemea pressure ya mitandaoni. Kelele za uchaguzi ule ndio hizi zinafanya viongozi waliopewa nafasi kwa uchaguzi haramu wanaogopa hata kuitisha mikutano, na wanaofanikiwa wanatumia nguvu kubwa, fedha nyingi nk. Sikuona nidhamu kipindi cha dhalimu, bali niliona sifa za kijinga, kusaka kiki na propaganda mfu. Yote haya tunayaona kwa macho yetu. Usidhani kila mtu alitekwa na zile taarifa na sifa za kupika.
Hivi wewe upo Tanzania kweli? Hebu tuanzia hapo kwanza.
 
Sasa kuna mtanzania halisi ambaye atatimiZa wajibu wake bila kushurutishwa?
Jamaa wanaongea vitu vya kufikirika tu, ndio maana nimesema huyo Jiwe hakuikuta hiyo sijui nidhamu ya kutoka moyoni anayoiongelea Samia.
 
Kwamba hii mijadala yenu humu mitandaoni inaipa pressure serikali hii ya ccm? Nimemwambia anitajie jambo moja tu ambalo wabongo mliipa pressure serikali kutokea humu mitandaoni ila hakutaja hata moja.
 
Mifumo ndio inapaswa kubana watu, na sio rais kufoka kwenye majukwaa ya siasa.
Vitu vyengine ni kujijengea utamaduni tu maana sisi sio mang'ombe, na ndio tofauti ya waafrika na wenzetu ngozi nyeupe.
 
Back
Top Bottom