Kwani Samia anapangiwa labda na Kikwete tu ila Ndugai kutoa maoni pinzani tu kamshughulikia.
Nimekuelewa,
Ni kweli Ndughaii aliongea jambo sahihi kabisa,
Tena hata kwa mujibu wa Katiba inaruhusiwa mwananchi kutoa maoni yake juu ya jambo lolote lile.
Lakini kwenye swala la Ndughaii kuna la kujifunza,
Unajua ukiangalia kwa macho ya rohoni kilichomtokea Ndughaii huenda ni adhabu na malipo ya yale alokuwa akiwafanyia wengine [emoji108]
Madam ametumika tu na Mungu kumuadhibu lakini ile huenda ilikuwa ni matokeo ya vile alivyowafanyia wengine.
Imeandikwa: ajikwezae atashishwa, ajishushae atakwezwa.
Pia Imeandikwa; Mungu humpinga mwenye kiburi.
Unajua kanuni mojawapo ya rohoni iko hivi;
Ukimuonea mtu au humuumiza mtu sababu ya madaraka yako, pesa yako, n.k ujue Mungu atainua mtu mwingine mwenye nguvu au pesa au madaraka zaidi yako akushughulikie ipasavyo [emoji108][emoji108]
Na wakati mwingine Mungu huamua kuingilia kati mwenyewe kwa kutimiza mapenzi yake!
Kwa hiyo tuishi na watu wote kwa wema na haki.
Yani kwa kufanya hivyo Mwenyezi Mungu atamu- establish na kinyume chake mtu huyo muovu huondolewa kwenye kile anachotegemea matharani madaraka, pesa, nguvu n.k
Yani hata kama unataka kumuadhibu mtu muadhibu kwa haki ambayo ipo kisheria na kuzingatia utu pia.