Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Rais Samia amewaonya vikali wateule wake, aliowateua majuzi, kuwa wasitumie madaraka yao kupiga "dili" za pesa, badala yake akawaambia ya kuwa wanatakiwa kufanya kazi Kwa weledi mkubwa na kuwatumikia wananchi Kwa uaminifu mkubwa.
Aliyatamka hayo maneno wakati akiwaapisha jana jijini Dar.
Rais Samia ametoa onyo Hilo muhimu sana Kwa wateule wake, Kwa kuwa hivi sasa, wateule wengi wa Rais, wanapopewa fursa kama hizo, wanachofikiria wao ni kujitajirisha Kwa kiasi Cha kutisha Kwa kutumia dhamana ya ofisi hizo za Umma
Akaendelea kuwapigia "mkwara" wateule wake hao kuwa hivyo vyeo, alivyowapa ni sawasawa na koti la kuyazima, wakati wowote anaweza kuwanyang'anya
Ukitafakari Kwa makini, maisha wanayoishi hao mawaziri ni ya fahari kubwa, ambayo hayalingani na kipato Chao Cha mishahara!
Wanachofanya hao mawaziri ni kama wako Kwenye mashindano ya "kuzipiga" pesa za Umma, utadhani wapo katika mashindano ya olimpiki!😀