Rais Samia awapa shavu Wazanzibar: Ajira asilimia 21 za Muungano kuwa za Wazanzibar

Halafu wakipewa kazi wanafika kazini saa tano mchana na ijumaa wanafunga ofisi
 
Hapa namuunga mkono Samia kwa kufanya HAKI bin HAKI huu Muungano tuliingia kwa lengo la kuwameza Wazanzibari sasa Mungu katugeuzia Kibao😂😆

Kwa hakika akandamize hapo hapo na akiongeza itapendeza zaidi 😁😁
 
Ulitaka wasipewe

79 kwa 21

Hizi roho mbaya Jamani tuzitafutie dawa yaani hii ni Zaidi ya Uchawi

Katika 79 kuna 21 Ngapi?

Kwani katika 60m kuna 1.5m ngapi?

Wewe hujui kwanini mapendekezo ni kuwa akandamize zaidi hadi akili nawe ikiungie?

"Mama Samia kandamizi 50/50 au zaidi bado misukule tupo hatujakusoma 😁😁."
 
Niko Zanzibar mwaka wa kumi Sasa Kila nikiomba kitambulisho cha uzanzibar mkaaz naambiwa Sina sifa hivyo siwez kuajiriwa Wala kumiliki ardhi Zanzibar cha ajabu wazanzibar Tamisemi wakitoa ajira wanaomba na wanapata vizur tu achilia mbali hizo ajira za Jw, polisi, uhamiaji na ardhi pia bara wanamiliki Bila bugudha , hii sio haki kabisa.
 
Muungano huu wa kipuuzi ulitokana na mawazo ya mtu mmoja tu(Nyerere) na kwa ubwege wa viongozi wengine wa wakati huo walivyokuwa wanamuogopa walishindwa hata kutoa ushauri wa kuweka kipengele cha kufanya majadiliano upya angalau kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na mahitaji ya wakati huo matokeo yake ndio haya sasa tunaishia tu kulalamika lakini hakuna mlango wa kutokea.
 
10 tena kwa mama Sukuma Gang waisome namba vizuri.
Mungu amejibu maombi ya upinzani .
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani kwenye mikataba tunavyoliwa. Kama Zanzibar tu inatushinda kunegociate nao kenye kugawana ajira eti kesho kuna mtu ataamini tumeweza kwenye Bandari ya Bagamoyo ....!!
 
It is their time babeee....

Mama songa mbeleee
 
Hapa namuunga mkono Samia kwa kufanya HAKI bin HAKI huu Muungano tuliingia kwa lengo la kuwameza Wazanzibari sasa Mungu katugeuzia Kibao😂😆
Yani mi nabariki kabisa...

Wacha tuvune tulichopanda.
 
Basi muungano uvunjwe na kuwe na nchi moja ya Tanzania, rais mmoja , Zanzibar kusiwe na rais ila ubaki kama mkoa ,
Hapo ndio hawatokubali kabisa yani wajitoe hadhi yao ya kitaifa wabakie kuwa mkoa, hilo hawatotaka
 
Kama sikusahau Marehemu Mtikila aliwahi kusema kuwa Nyerere aliiuza Tanganyika kwa Wapemba!
 
Zanzibar nchi ndogo ina watu wachache lakini ina serikali yake, ajira katika hiyo serikali ni. za wazanzibar pekee.
Zanzibar ardhi yake ni kwa ajili ya Wazanzibar peke yao

Ila ardhi ya Tanganyika ni ya WOTE including wazanzibar.

Ajira za Tanganyika kwenye mambo yasiyo ya muungano ni ya WOTE including Wazanzibar.

Sasa huu muungano gani wa Chao chao, chetu chao?
 
Hata Mimi nawashangaa Watanganyika wenzangu. Hii asilimia 21 iliwekwa na awamu ya 4. Awamu ya 5 wakagoma kuitekeleza. Huyu hangaya wanamuonea bure tu.



upuuzi huu uliafikiwa kwenye kikao hicho hapo juu wa maelekezo ya mama maushungi na wala sio kipindi cha awamu ya 5
fuatilia yaliyoafikiwi kwenye hicho kikao kuna maupuuzi mengi sana ya kuwapendelea wanzazibar ndio maana hata yaliyojiri yalifichwa .
moja wapo ya maafikiano ya kikao hicho ni huu upuuzi,wa ajira ila yapo mengi sana,

jafoo na mr planning ni watu wapuuzi sana
 
Wapinzani hawachoki kuibua mambo wakishindwa hili wanaibua lile. Wao walitaka serkali tatu ambayo kila mtu angebaki kwao, ikakataliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…