Rais Samia awapa shavu Wazanzibar: Ajira asilimia 21 za Muungano kuwa za Wazanzibar

Rais Samia awapa shavu Wazanzibar: Ajira asilimia 21 za Muungano kuwa za Wazanzibar

Magufuli alichukua Wasukuma wenzake na kuwajaza kila sehemu, sasa ni zamu ya Wazenji kujazwa kila mahali

Mtu mzima kuwa mropokaji haipendezi! Wasukuma kwa idadi tu ni zaidi ya Wazanzbar wote sasa compare kwenye suala la ajira alilo semea Misile
 
View attachment 2015004

Watu milioni 58 wanagombania asililia 79 ya Ajira

Ila watu milioni 1.5 unawapa asilimia 21 ya Ajira

Hongera mama, Charity begibs at home.

Watanganyika huu ni muda wa kukaa na kutafakari huu muungano una faida na sisi au la?

Hebu tazama

1. Mzanzibar ana haki ya ardhi yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ila wewe Mtanganyika unaweza kupata ardhi kwa masharti ya wageni

2. Mzanzibar anahaki na Ajira zote za mambo hata yasiyo ya muungano kwa mfano TAMISEMI

3. Mzanzibar anaweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi huku Tanganyika hata kwa mambo yasiyo ya muungano kwa mfano balozi wa nyumba kumikumi lakini Mtanganyika hawezi kuwa shehia kule Zanzibar

4. Ajira zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni exclusive kwa ajili ya Wazanzibar, Yaani Wao wanakula kotekote Tanganyika na kule Zanzibar

5. Wao wamepambana kuondoa mafuta kwenye mambo ya muungano, lakini sisi Ardhi yetu wanaitaka, na wanaienjoy sana tu kwa sababu nawajua Wazanzibar wanaomiliki ardhi TZ

Sasa katika hali kama hii, Huu muungano una faida kwa Watanganyika kweli
Hizo ajira wenyewe zipo?
 
Thread za UCHONGANISHI.

Hivi Kati yenu na mwalimu Nyerere nani ni mzalendo zaidi?

G55 mlishakufa mmefufuka?!

Siempre JMT
Nchi Kwanza
 
Asilimia 21 ni kubwa sana, ilitakiwa wapewe asilimia moja au 0.95, huu ni wakati wa watanganyika kuamka na kudai serikali ya Tanganyika kama ilivyo serikali ya zanzibar, ratio ilitakiwa igawiwe kutokana na idadi ya watu
Serikali ya Tanganyika haipo na haitokuja 🤣🤣
 
Huu muungano hauna maisha marefu, muungano una mambo mengi ambayo hata ukimusimulia mtoto wa darasa la kwanza atashindwa kuelewa kwanini hivi. kuna siku kitanuka
Muungano wetu ni wa kipekee, huyo mtoto msimulie kwa kumwambia kuwa "huu ni wa kipekee"

Hasta la Victoria El Comandante JKN🙏

SIEMPRE JMT
 
Duh sina neno sahihi la kuandika,huu ni zaidi ya upuuuuuuuuuuuuuuuuuzi.
 
Halafu cha ajabu, ikitangazwa kazi inayohusu mambo yasiyo ya muungano, bado wazenji wanaapply na hawawekwi pembeni sababu ya uzanzibar wao, Wanakuwa treated sawa na vijana wa Tanganyika.
Wapo watendaji wa serikali za Mitaa huku bara ni Wazanzibar, japo TAMISEMI siyo jambo la muungano!
Muungano wetu ni wa kipekee.

Hayati JKN alikuwa na fikra na upeo wa mbali mno zaidi ya "wanaharakati" wa siku hizi

Hayati JKN alilijua hilo kuwa WAZANZIBARI si watu wa kutoka AUSTRALIA huko bali wengi wametoka huku bara, sasa utaifa wao ni jambo la "kiprotokali" baada ya kuupata Uhuru wao

Hayati JKN atabaki alama ya kuupinga UMIMI NA SIASA ZAKE, bahati mbaya baadhi ya WANASIASA na WANAHARAKATI wanauangalia muungano KIWEPESIWEPESI NA KIFITNAFITNA

Muungano huu wa kipekee utadumu na kushinda sababu koko na nyepesi.


HASTA LA VICTORIA EL COMANDANTE JKN🙏

SIEMPRE JMT🙏

KAZI IENDELEE 🔥🔥💪💪
 
Heshima sana wanajamvi,

Leo nimemsikia Waziri wa Utumishi na Utawala Bora akisisitiza juu ya mgao wa ajira 21% Zanzibar.Suala hili pamoja na makando kando yake ya upendeleo wa wazi kabisa nafikiri pia wakaazi wote waliopo ukanda wa pwani 10 kilometa wangenufaika na upendeleo huo tukianzia Lindi, Dar, Tanga, Mtwara na & Pwani.

Sasa ni wazi ipo sera ya upendeleo wa sehemu atokayo Rais kumbe tulikuwa tunamlaumu bureeeee Bwana yule.

Nawasilisha Povu ruksa.
 
Sijui mwalimu wangu Nguruvi3 yupo wapi siku hizi.

===

Jaji Warioba anasema tubadili muelekeo wa kuwaanda vijana wetu kuvizia kazi za serikalini.
 
Hiyo ratio ya 21% ilikokotolewaje? kama sio 1.5x100/60 =2.5, basi Wazanzibari wanafaidi
 
Ulitaka wasipewe

79 kwa 21

Hizi roho mbaya Jamani tuzitafutie dawa yaani hii ni Zaidi ya Uchawi

Katika 79 kuna 21 Ngapi?
 
  • Thanks
Reactions: Eco
Back
Top Bottom