Rais Samia awashangaa wanaosema miradi ya Magufuli haitoendelezwa, adai uwezo wao wa kufikiri ni mdogo

Rais Samia awashangaa wanaosema miradi ya Magufuli haitoendelezwa, adai uwezo wao wa kufikiri ni mdogo

Kiturilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
708
Reaction score
2,859
Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli haitaendelezwa, hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo, zilizojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016.

“Kulikuwa na maneno mengi, iliyoachwa haitaendelezwa ukiuliza sababu hakuna. Hakukuwa na sababu ya kwamba miradi hiyo isiendelezwe, kwani ilianzishwa na kuagizwa ndani ya Ilani ya CCM. Sasa kwa kunitazama sura na kusema isingeweza kutekelezeka miradi nadhani hekima haikutumika.

“Wanaposema miradi haitaendelezwa nadhani upeo wao wa kufikiria ni mdogo sana. Hata miradi hii ilivyoanzishwa nilikuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo ni sehemu tangu kuanza kwake na kutekelezwa,” amesema Rais Samia wakati akizindua mradi wa nyumba 644 za Magomeni Kota.

Hata hivyo, Rais Samia akiwahutubia wakazi wa Magomeni na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam amesema “lakini tuwaombe nasi tujiombee kwa Mungu atupe nguvu, uwezo na hekima zaidi ili tuweze kuendeleza miradi kwa maendeleo ya Taifa.
 
kila siku kuongea yale yale tu, inamaana hana sera, kuna watu anashindana nao au? 2025 ije haraka tu tupate Rais mwingine huyu hapana kwakweli
Huyo Rais mwingine nae akiwa anaongea yale yale (kwa mujibu wa madai yako) utataka pia aje tena mwingine? na huyo mwingine yeye hatakua na mapungufu yake ya kibinadamu?
 
Tanzania imepita marais 5 ila yenyewe ipo na itaendelea kuwepo baada ya mh.Rais Samia na watakaomfuatia.....

Twende na mh.Rais SSH kwa ujenzi wa Tanzania bora!!!!

#Siempre JMT🙏
 
Muhimu hayo majengo wahusika wayatunze na kuyathamini,sio baada ya muda mfupi tu yawe yanaonekana kama majengo yaliyojengwa miaka mingi kwa kukosa matunzo.
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi......👊👍👏💪

#TanzaniaIpoMilele
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli haitaendelezwa, hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
😍
 
Back
Top Bottom