Kwa nini hatilii mkazo miradi mkakati kama JNHP ambao ni mradi utaosaidia kuondoa dhahama na matatizo kwa watanzania wa kila namna?
Mradi wa Sgr anauchungulia kama vile ni mradi usio na tija kabisa. Yupo busy na kusafiri na kucheza filamu kama Royal tour ambazo hazina tija kwa taifa wala mwananchi wa kawaida.
Kuna upungufu mkubwa wa huduma za afya maji na na elimu na sisi kama taifa bado tupo nyuma sana. Kwa nini mkuu wa nchi hajatilia mkazo juu ya hii kero zaidi ya Royal tour isiyo na tija kabisa?