peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
07 November 2022
Sharm El Sheikh, Egypt
MKUTANO WA COP27 SHARM EL SHEIKH EGYPT 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na wakuu wengi wa nchi wapo kuhudhuria Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu 2022 unafanyika mjini Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
Ajenda kuu ni kunusuru ulimwengu ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa / UN Bw. General António Guterres amepeleka ujumbe kwa dunia kuwa mpaka sasa ktk mapambano ya kunusuru uhai wetu, tunaelekea kushindwa.
Katibu mkuu wa UN Bw. António Guterres anaongeza tupo katika spidi kali barabara kuu kuelekea mazingira ya hali ya hewa ya kuzimu huku tukikandamiza vikali accelerator ya mwendo wa gari . Maneno hayo mazito yanaashiria kuwa inabidi dunia kuchukua hatua za ziada kupunguza uharibifu wa mazingira unaoleta mabadiliko ya tabia nchi .
Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Egypt nchi ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa TabiaNchi amesisitiza kuwa dunia yote inawaangalia viongozi wanaohudhuria mkutano huo waje na mkakati unaoweza kukabiliana na tishio la mabadiliko la tabianchi.
Mkutano huu utakuwa na vikao vingi vya wakuu wa nchi kukubaliana utekelezaji wa mkakati wa makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi, usipozingatiwa basi unaotishia uwepo wa maisha ya binadamu, ekolojia na viumbe duniani
Huyu mama haonagi aibu.
Huku ndege imeanguka.
Huku mlima unawaka moto.
Huku Hakuna maji
Huku Hakuna umeme
Huku mchele, mahindi, maharagwe kimekua chakula cha anasa.
Huku Wanafunzi wamekosa mikopo ya elimu ya juu.
Huku polisi wanapunjwa Malipo yao.
Bado anapita nchi kwa nchi?
Kweli Mtanikumbuka