Rais Samia awataka majaji, viongozi kuwa waadilifu ili Zuhura asiwahusu saa nane usiku

Rais Samia awataka majaji, viongozi kuwa waadilifu ili Zuhura asiwahusu saa nane usiku

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka majaji wapya aliyowateua hivi karibuni na viongozi wengine wa kiserekali kisha kuwaapisha leo kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na uaminifu.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama Kuu na Rufani pamoja na viongozi wengine aliyowateua hivi karibuni.

Amesema viongozi hao kila mtu kwa nafasi yake wanapaswa kuwajibika ili uepuka kutenguliwa nyadhifa zao saa nane za usiku.

“Natarajia wote mtakwenda kufanya majukumu yenu kama mlivyopangiwa, kwa upande wa mahakama kuko vizuri ila kwa wale wengine nikigundua kuna ili na lile basi Zuhura anawahusu saa nane usiku ndio utoa taarifa alfajiri ukiamka hakuna kitu,” amesema Rais Samia na kuongeza

“Tusifike huko nendeni mkawajibike kila mtu kwa nafasi yake ili Zuhura asiwaone, natarajia wote mtakwenda kufanya majukumu yenu kama mlivyopangiwa,” amesema

Credit:; Bongo 5
 
Kwa hiyo zuhura akiwaona tu huko wamekwisha! Kwani zuhura ndiye anayewateua? Au kazi yake ni kuwatengua akiwaona huko?
 
Back
Top Bottom