Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa jamii zinazoishi maeneo yenye vivutio vya Utalii, kuendeleza mila na desturi za maeneo hayo ili kulinda heshima ya mila hizo na kuendelea kuvutia utalii.
Rais Samia ametoa wito huo leo, wakati akifunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi, ambayo yamehusisha Sanaa, Utalii, Uvuvi, Ufugaji, Kilimo na Ujasiriamali, katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi Visiwani Zanzibar.
Amesema katika baadhi ya maeneo, Wenyeji hususani Vijana wamekuwa wakiiga utamaduni wa Wageni, hali ambayo inapelekea hata Wageni kuona hakuna jipya katika maeneo hayo.
Amesema Utalii ambao nchi inauhitaji, ni Utalii wenye kudumisha tamaduni, mila na desturi za Wenyeji, kwani ndivyo ambavyo huwavutia Wageni kutoka Mataifa mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia Mtindomaisha wa Wenyeji.