Rais Samia awateua Dkt. Mpango na Kassim Majaliwa kuwa washauri wake

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ya kimkakati katika safu ya washauri wake, akiwateua aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, na aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa Washauri wa Rais.

Akizungumza leo, Januari 10, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Rais Samia amefafanua kuwa Dkt. Mpango atakuwa mshauri wake katika masuala ya uchumi na miradi, wakati Kassim Majaliwa atakuwa mshauri katika masuala ya kijamii.

Rais amesema amemhamisha Profesa Palamagamba Kabudi kutoka Wizara ya Michezo na kumteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), ili kuratibu na kufanya kazi kwa karibu na washauri hao wapya.

“Pale Ikulu nahitaji akili iliyopevuka yenye maarifa mapana, yenye uzoefu mkubwa na mtu ambaye yuko vizuri kwenye kujieleza na kueleza jambo likaeleweka. Nimepiga picha serikalini kwangu kote nikasema Profesa Kabudi atanifaa”, amesema Rais Samia akielezea sababu za kumrejesha Prof. Kabudi Ikulu.
 
Duh!...
 
Screenshot_20251222-120716~2.png
 
Angekua anapenda ushauri angechukua ushauri wa polepole,gwajima au hata lissu kabla ya uchafuzi mkuu walau angeliepusha taifa na fedheha tuliyoipata

Ujinga mtupu....Simbachawene ameshauri vizuri na akataka kumaliza mzizi mzima wa chuki kati ya polisi na wananchi lakini Samuya hakupenda KAMFUKUZA.
Hamjui Tanzania anayetakiwa kushauriwa ndiye anakuwa mshauri kwa washauri wake?
 
Kujaribu ku-balance. 1. Ilisemekana Majaliwa na Mpango waliamua kumwachia kutokana na maovu yaliyokuwa yanafanywa... 2. Mitaani wananchi wakawapongeza M.M kwa kutogombea. 3. Lawama zote akapewa yeye na kuitwa king'ang'anizi. 4. Anawarudisha kwa kuwatangaza ili wanuke wote. Kwani alikuwa anaweza kuwaomba ushauri (kwa nafasi zao kiutumishi ktk taifa) BILA MATANGAZO.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ya kimkakati katika safu ya washauri wake, akiwateua aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, na aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa Washauri wa Rais.

Akizungumza leo, Januari 10, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Rais Samia amefafanua kuwa Dkt. Mpango atakuwa mshauri wake katika masuala ya uchumi na miradi, wakati Kassim Majaliwa atakuwa mshauri katika masuala ya kijamii.

Rais amesema amemhamisha Profesa Palamagamba Kabudi kutoka Wizara ya Michezo na kumteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), ili kuratibu na kufanya kazi kwa karibu na washauri hao wapya.

“Pale Ikulu nahitaji akili iliyopevuka yenye maarifa mapana, yenye uzoefu mkubwa na mtu ambaye yuko vizuri kwenye kujieleza na kueleza jambo likaeleweka. Nimepiga picha serikalini kwangu kote nikasema Profesa Kabudi atanifaa”, amesema Rais Samia akielezea sababu za kumrejesha Prof. Kabudi Ikulu.
View attachment 3527982
Anataka ashauriwe nini kama kila ushauri wenye tija haukubaliki kwake?
 
Kujaribu ku-balance. 1. Ilisemekana Majaliwa na Mpango waliamua kumwachia kutokana na maovu yaliyokuwa yanafanywa... 2. Mitaani wananchi wakawapongeza M.M kwa kutogombea. 3. Lawama zote akapewa yeye na kuitwa king'ang'anizi. 4. Anawarudisha kwa kuwatangaza ili wanuke wote. Kwani alikuwa anaweza kuwaomba ushauri (kwa nafasi zao kiutumishi ktk taifa) BILA MATANGAZO.
Kikwete anayemshauri mbona hamtangazi, wazee wa watu wamepumzika anataka wanuke wote.
 
Back
Top Bottom