Rais Samia awateua Lukuvi, Bulembo, Balozi Luhwavi na Omar Kheir kuwa Washauri wa Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii

Rais Samia awateua Lukuvi, Bulembo, Balozi Luhwavi na Omar Kheir kuwa Washauri wa Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-

(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(in) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

View attachment 2656461
Kazi kweli kweli,Mama ameanzisha kitengo cha siasa na mahusiano ya Jamii.Wapi Ofisi Kuu au Kwenye Chama.Kwa nini uteuzi huu umefanyika mara moja baada ya Mahakama ya haki za binadamu na utawala borra kutoa zuio la Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya kutopisha wa CCM bila kupingwa.Hukumu ulitakiwa kuwe na zuio la Wakurugenzi kutokuwa returning officers wa uchaguzi.Tume ya Uchaguzi itoe. Ajira kwa vijana wetu ambao hawana Kazi
kuwa returning officers na wasaidizi wao.Hizo ndiyo gharama za demokrasia
 
Lukuvi ni usalama wa Taifa, atatumika popote Rais atakapoona inafaa.
Hivyo?

Ina maana hawa watu wa usalama wao akili kichwani hawana, ni kama ma-robot tu ya kutumikishwa basi?

Mbona ingekuwa ni kweli hayo unayoyasema, ndiyo ingekuwa nafasi nzuri kabisa ya kulinda usalama wa taifa? Au hlli siku hizi lina tafsiri tofauti?
 
Ni wazo zuri kuwa na washauri wa karibu ukiwa kiongozi.

Swala Hawa washauri wanajuwa maisha yetu huku kwa kajamba nani au watahusika na wale wenye maisha ya kati na juu?

Kwa kajamba nani ndipo Wadanganyika tulipojazana, tuna imani watatufikia na kuwasilisha maoni na shida zetu.
 
Upuuzi mwingine tena; hivi kweli lukuvi ambaye anachojua ushirikina tu na huyo bulembo jamani, kweli kabisaaaa, sasa wanahusianisha nini na kwa kipi. Labda kwakuwa ile sherehe yake ya mwanza na waganga wenzie wajadi ilisukuma huo uteuzi. NCHI INA LAANA hiyo.
 
Upuuzi mwingine tena; hivi kweli lukuvi ambaye anachojua ushirikina tu na huyo bulembo jamani, kweli kabisaaaa, sasa wanahusianisha nini na kwa kipi. Labda kwakuwa ile sherehe yake ya mwanza na waganga wenzie wajadi ilisukuma huo uteuzi. NCHI INA LAANA hiyo.
🤣😂😅
 
Makafir most of
Sawa kamchomekea Mzee Lukuvi, ila tunajuaaaa kamchomekea Kwa makusudi na Wala hampendi.



Siku akijifunza Kusimama kwenye haki, Akaachana na Uswahili ,na Uislam, atafaa japo ameshachelewa.




Nimshauri tu, aondoe wazi la kugombea.



Hivi kweli BULEMBO naye, ni wa kua mshauri wa Rais?? Huyu BULEMBO huyu jambazi la Mali za CCM?? .


Alafu hapo Rais anajiona salama?.


Mnajua Pengine, Rais Wetu Kawa blackmailed ila sisi hatujui , hivi ni Akili yake kabisa???.
Makafir most of you mna choko choko sana, uislam unawapa kimuhe muhe sana
 
Back
Top Bottom