Rais Samia awateua Lukuvi, Bulembo, Balozi Luhwavi na Omar Kheir kuwa Washauri wa Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii

Rais Samia awateua Lukuvi, Bulembo, Balozi Luhwavi na Omar Kheir kuwa Washauri wa Rais Siasa na Uhusiano wa Jamii

Bashiru hawez kununua Kwa sababu Moja ana akili Kubwa, pili msomi, tatu mzalendo.


Sanasana anaweza sikitika Kwa namna mambo yanavyoenda ,nayeye ni mzalendo.
angekuwa mzalendo angechukua rushwa wakati akiwa katibu mkuu wa chama? waulize wabunge watakwambia vizuri walikuwa wanampa ngapi yeye na polepole ili majina yao ya rudi.
 
Hilo ndilo lengo lake kuu. Siyo kweli anauhitaji ushauri wa Lukuvi bali anataka kumdhibiti, asiwe na uhuru wa kukosoa chochote.
Kumdhibiti Lukuvi tena?! hakuna kitu kama hicho, anajua kwenye hili la bandari ameharibu sana, anachofanya sasa ni kuunganisha yale makundi aliyoanza kuyatenga mwanzo ili apunguze lawama dhidi yake.
 
Sawa kamchomekea Mzee Lukuvi, ila tunajuaaaa kamchomekea Kwa makusudi na Wala hampendi.



Siku akijifunza Kusimama kwenye haki, Akaachana na Uswahili ,na Uislam, atafaa japo ameshachelewa.




Nimshauri tu, aondoe wazi la kugombea.



Hivi kweli BULEMBO naye, ni wa kua mshauri wa Rais?? Huyu BULEMBO huyu jambazi la Mali za CCM?? .


Alafu hapo Rais anajiona salama?.


Mnajua Pengine, Rais Wetu Kawa blackmailed ila sisi hatujui , hivi ni Akili yake kabisa???.
Bulembo ndio alikuwa campaign manager wa Mtakatifu Magufuli.
 
Yaani kwamba Lukuvi anadhiki sana, akikosa uteuzi huo maisha yake yanakuwa hohehahe?

hapa ndipo wanasiasa wa Tanzania wanapopotezea hadhi ya kuwa wanasiasa wa kweli. Inakuwa kama hawana lolote wanaloliamini maishani mwao. Hawana 'conviction' yoyote!

Katika hali ya namna hii iliyopo sasa utakuwa mshauri wa aina gani, kama siyo kutafuta kutumia jina lako tu wajisafishe na madudu waliyoyatengeneza wao?

Lukuvi kaondolewa kwenye wizara aliyoimudu vizuri kabisa. Alipewa sababu zipi z kumpumzisha katika kazi iliyokuwa inakwenda vizuri?
Lukuvi ni usalama wa Taifa, atatumika popote Rais atakapoona inafaa.
 
Washauri wa Rais hulipwa mishahara au kazi ya kujitolea tu?

Bulembo atashauri nini cha maana ilhali yeye mwenyewe anahitaji washauri binafsi!

Yule na Mzee Makamba ni kasoro tarehe tu.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-

(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(in) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jami). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Maji yanazidi kuongezeka kina, yatafika mabegani soon
 
Back
Top Bottom