Rais Samia awatumbua Mkuu wa Wilaya Morogoro Bakari Msulwa na Mkurugenzi Morogoro Sheilla Lukuba Kwa Mgambo Kuwapiga Wamachinga

Kwahio alingoja kuwatumbua leo wakati kosa lilifanyika lini ? (au alikuwa bado anafanya upelelezi kuhusu makosa na jibu alipata dakika chache kabla ya utumbuzi)?

Nilidhani hizi zama zimekwisha....
 
Anataka kutuletea akina Sabaya tena?
 
Namuombea paskali kwa mungu safari hii awe DC na mama atanifurahisha akimtumbua DC wa arusha maana hana tofauti na sabaya
 
Umesahau mama yetu samia haui watu
 
Mwenyezi Mungu awape subira!

Labda kama kuwe na makosa au tuhuma nyingine mbali na hiyo kadhia ya machinga lakini kama sababu ni hiyo tu kwa kweli mmh !
 

Busara ilitakiwa kutumika, hawa sio majambazi kama sabaya, kuwasikiliza kwanza, maybe they have a sensible defense. Mimi sio muumini wa huu upuuzi.
 
Sasa kuna sababu gani ya kutumbua mtu wakati unakaribia kufanya mabadiliko nchi nzima.
Sijui kama amejiridhisha bila shaka, kuwa viongozi hao, ndio waliwatuma mgambo kufanya hayo, ama unakuta ni viongozi walio chini yao tu waliamua 'kujimwambafy wenyewe' dizaini ya jamaa yetu wa Hai.... kaaazi kwelikweli. Na kweli kazi iendelee.
 
Nataka kufanya application ya udc au ukurugenzi, nifanyaje, nipate chance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…