Rais Samia awatumbua Mkuu wa Wilaya Morogoro Bakari Msulwa na Mkurugenzi Morogoro Sheilla Lukuba Kwa Mgambo Kuwapiga Wamachinga

Rais Samia awatumbua Mkuu wa Wilaya Morogoro Bakari Msulwa na Mkurugenzi Morogoro Sheilla Lukuba Kwa Mgambo Kuwapiga Wamachinga

Wakufukuzwa walikuwa madiwani na baraza lao.
Barabara za Morogoro wanakojirundika ni finyu SANA. Nyembamba na kuna vurugu za bajaj na bodaboda... Kwa hili mama Rais kakurupuka angechunguza zaiidi kwanini manispaa iwe na msimamo huo.!
Roundabout ya mjini kati wakirudi, iko siku watagongwa watu, kisha tuwatumbue wengine.

MASOKO mengine yanayokusanya mapato na halmashauri yatakosa wateja sasa hivi!

La sivyo wakubaliane na TARURA ile iliyokuwa stendi ya hiace ya zamani, liwe soko..
Huu utitiri wa vijisoko kila baada ya mita 200 Morogoro ni mpango wa kipuuzi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
20210524_223453.jpg

Namuona Devotha Minja anavyomkumbusha mkurugenzi na mkuu wa wilaya Yale madhila waliyomtendea kipindi Cha uchaguzi wa 2020! Karma ipo na inawinda kila sekunde!
 
Kwahio alingoja kuwatumbua leo wakati kosa lilifanyika lini ? (au alikuwa bado anafanya upelelezi kuhusu makosa na jibu alipata dakika chache kabla ya utumbuzi)?

Nilidhani hizi zama zimekwisha....
Kuna maeneo tuwe wakweli, hii siyo sawa.
Nchi Ina Sheria za mipango miji Kama nchi itaendeshwa kwa siasa na uholela ivi hatutakuwa na miji Safi Bora na yenye mpangilio.

Kama ndivyo idara ya mipangomiji ifutwe tuokoe pesa ya kuwalipa watumishi wa idara hiyo nchi nzima maana haina kazi
 
Mipango miji itasaidia nini kama wananchi wataendelea kuteseka, Bora tunyanganyane hicho kidogo kilichopo
 
Shida Chuki zimezidi mkuu!
Baadhi hata hawakukosewa hata hawaelewi lipi ni baya kwa Magufuli ila wanaambiwa nyumbani mambo hayo! Ndo maana nilimuona Mbowe kama hazimtoshi baada ya kujiita shujaa wa kusema jambo la ukabila bila hata ushahidi.
 
Leo asubuh DC alikua redio Iman anazungumza km machale hv nikasema hyu sijui n he didn't see it coming.
 
Back
Top Bottom