RAIS SAMIA SULUHU ATUMBUA WAKURUGENZI WANNE WA HALMASHAURI...AMUWEKA KIPORO YULE WA GEITA,
======
RAIS Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Februari 4, 2022 akiwa njiani Magu jijini Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara,
Rais Samia ametengua uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini,
Wakurugenzi hawa wanakabiliwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa mapato katika halmashauri zao,
“Siku ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi yangu halisi achezee hizo fedha "
Rais Samia Suluhu amesema traarifa zilizopo, Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha.
" Mheshimiwa waziri (Waziri wa Tamisemi) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi” amesema Rais Samia na kuongeza
“Yule wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa” amesema
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo mengine.
Waziri Bashungwa alianza kwa kutoa pongezi kwa Rais Samia kutokana na ujenzi wa madarasa ya fedha za Uviko-19.
Baada ya kumaliza, Rais Samia alimuagiza Waziri Bashungwa kutaja maeneo mengine ambayo kumefanyika ubadhirifu.