Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Kamati za mipango ya matumizi ya pesa hizo zinapangwa na kusimamiwa na afisa maduhuli. Walimu wakuu wanaweza wasiwe hata kwenye mpango wa matumizi
 
Hawa ni vijana wa JPM wote
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa...
Mtoto wa Jaji Luvuba mzee alisaidia CCM kuingia madarakani
 
Hao kosa lao itakuwa wamekula wakavimbiwa, Rais hapendi hilo anataka ule kwa kiasi.

Huyo mkurugenzi wa Iringa sio yule alieshutumiwa kwa ubakaji siku chache zilizopita? kama ndie akapumzike tu, yeye alikuwa hachagui vyakula anabugia chochote.
Ndiyo huyu alimnyanyasa binti ambaye ni memba hapa JF
 
Anatumbuliwaje mtu kwa sababu tu ya tuhuma? Je tuhuma zikishindwa kuthobitishwa? Namkumbuka yule Mkurugenzi aliyechongewa na mbunge wake kuwa kajinunulia Vieiti kinyume na utaratibu! Mwisho wa siku ikagundulika kuwa alikuwa na baraka zote zilizotakiwa. Utumbuaji wa namna hii inawapa nguvu wale wanaopenda kuchonganisha na kuwaharibia watu.

Amandla...
 
kwakweli kama wamekula fedha za walipa kodi lazima washughulikiwe kwa mujibu wa Sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…