Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Usiombe kujikuta uraiani ghafla bin vuuuh!!

Pole sana kwao waliokuwa wakurugenzi , Hongera sana kwa Rais Samia kusimamia maslahi ya Taifa!

Liwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizo
Wanarudi kwenye kazi zao kabla ya kuteuliwa, na wanarudi na mishahara yao ya ukurugenzi, watakachokosa mi V8 na marupurupu manono.
Hawa jamaa wakirudi kwenye kazi zao za awali hawapendwi na maboss wao maana wanawazidi mishahara.
 
Yule wa bunda aliyejenga msingi kwa 60ml anasubiri nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
si alisema hatatumbua bali atawapa onyo kwanza imekuwaje hawa amewatengua?
 
DED wa mbeya mjini ametumbua pesa za UVIKO.

Gapo ni nyumbani kwa spika wetu Tulia. Hii imekaaje?

Muwe na weekend njema.
 
Likely huyo Limbe itakuwa ile mada iliyoletwa humu kuhusu kumbaka mtumishi aliyeenda kufuatilia issue yake ya bima.

Nafikiri kama ushahidi upo basi hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 
Halmashauri ya Buchosa ilikuwa chini ya Mkurugenzi Paulo Malala, Mkurugenzi wa Iringa ni Limbe B. Limbe, Mkurugenzi wa Singida Mjini ni Zefrin Kimolo Lubuva, na Mbeya Mjini ni Amede E.A Ngwanidako
Ha ha haaa! Wale wa kusema 'hakuna' maamuzi ya hadharani na papo kwa papo, kwani kufanya hivyo ilikuwa kiki, waje hapa tuwaone!

Hii ni kutaka mrejee tukio la mama aliyekuwa anafanya kazi huko kwenye 'hospitali maalumu' kisha akataka kukatisha mazungumzo ya haki.
 
Waandishi wa HABARI nchii hii mpo kimya sana hivi Ile ajali ya msafara wa mkuu wa mkoa mwanza sio alikuwa anapitia hii miradi iliyotafunwa na hao maded ,hao maded ni mafia sana unaweza Kuta waliogopa waandishi watawaumbua kwenye value of money ya kwenye miradi hiyo.
 
Hivi zaidi ya kufutwa kazi kuna hatua nyingine kama kushtakiwa na kupelekwa mahakamani wanayochukuliwa?
 
Wakafanye shughuli zao za zamani huku wakila mishahara mikubwa.
 
si alisema hatatumbua bali atawapa onyo kwanza imekuwaje hawa amewatengua?
Na siyo onyo!

Bali alisema atawaelekeza mara tatu, baada ya hapo anatumbua..

Sasa sijui imekuwaje tena?
 
Usiombe kujikuta uraiani ghafla bin vuuuh!!

Pole sana kwao waliokuwa wakurugenzi , Hongera sana kwa Rais Samia kusimamia maslahi ya Taifa!

Liwe fundisho kwa wengine wenye tabia hizo
Hao hawaji uraiani ni watumishi wa Umma watapangiwa kazi nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…