Rais Samia awazawadia Serengeti Boys, U17 milioni 500

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imetoa zawadi ya sh. milioni 500 kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano hayo na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo (Ijumaa, Mei 29, 2026) ofisini kwake Mlimwa, Dodoma wakati akitoa salamu za pongezi kwa timu hiyo kufuzu hatua ya fainali kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wote wa timu kwa mafanikio hayo makubwa ambayo yameendelea kuandika historia mpya katika sekta ya michezo nchini.

“Mheshimiwa Rais amenielekeza nitoe pongezi hizi kwa vijana wetu wa Serengeti Boys kutokana na mafanikio makubwa ya kutinga fainali na kuiwakilisha vema Tanzania katika mashindano hayo,” amesema Dkt. Mwigulu.

​
 
Hizi ni Hela zetu walipa Kodi? Au ni za wajomba zetu wa Arabuni?
Nyie nyumbu, yaani haters, mnatamani kusema vipi Ili nafasi zenu za kishetani zifurahi?!! Sema hivyo mioyo yenu inavyotamani, Haina shida kabisa kwa Jemedari wa vita, Dr Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania. Kwani kwake, nyie ni vichinda tu visivyomsumbua kwa lolote hivyo hawafikirii tu.
 
Tunatamani kusikia ame RIP
 
Aisee, Million 500 kwa kushinda mechi ya mpira na kuingia finally. Hiyo pesa haiwezi kurudi kivyovyote. Hakuna tangible Return of Investment. Kodi za wanachi zinakuwa wasted out of extravagance. Huku wasomi tangu 2017 hawana ajira na kujiajiri hawawezi sababu hakuno miundombinu. Juzi katoa millioni 200 za mkopo kwa vijana wenye njaa mitaani, lakini huku katoa 500 ndani ya dk 90.

Amefanya hivyo kusudi sababu anajua watanzania wengi ni vichwa maji na mpira ndio kimbilio lao baada ya kupigwa na jua mchana. Na walivyo wajinga watafurahia kwelikweli.
 
Pole sana kwa maumivu
 
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imetoa zawadi ya sh. milioni 500 kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano hayo na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo (Ijumaa, Mei 29, 2026) ofisini kwake Mlimwa, Dodoma wakati akitoa salamu za pongezi kwa timu hiyo kufuzu hatua ya fainali kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wote wa timu kwa mafanikio hayo makubwa ambayo yameendelea kuandika historia mpya katika sekta ya michezo nchini.

“Mheshimiwa Rais amenielekeza nitoe pongezi hizi kwa vijana wetu wa Serengeti Boys kutokana na mafanikio makubwa ya kutinga fainali na kuiwakilisha vema Tanzania katika mashindano hayo,” amesema Dkt. Mwigulu.

Waziri Mkuu amesema Serikali itatuma ndege maalum kwa ajili ya kuwafuata vijana hao watakapomaliza mashindano hayo ili kurejea nchini pamoja na kombe endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa. “Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege kwa ajili ya kuwafuata vijana wetu watakapokuwa wamemaliza mashindano hayo na kurejea nao nyumbani,” amesema.

“Tunaamini huu ni mwanzo tu wa pongezi ambazo Mheshimiwa Rais ameanza kuzitoa. Tunaamini kwamba wakirejea na kombe hilo, kutakuwa na sababu zaidi ya kuwapongeza kwa mafanikio hayo makubwa.”

Waziri Mkuu amemwelekeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda na wadau wanaohusika, waendelee na uratibu wa wa safari kwa watu watakaokwenda kuwaunga mkono vijana wetu.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema endapo Serengeti Boys watatwaa ubingwa, Serikali itawapatia kila mchezaji kiwanja kimoja katika Mji wa Suluhu New City uliopo mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuitangaza Tanzania kupitia michezo.

Waziri Mkuu pia amewahamasisha Watanzania, taasisi, mashirika na wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kutoa msaada na motisha kwa timu hiyo kuelekea mchezo wa fainali.

“Shime shime vijana wetu, inawezekana. Tuleteeni kikombe kile, mleteeni Dkt. Samia Suluhu Hassan kikombe, tuleteeni Watanzania ushindi huo. Kwa kiwango mlichokionesha, tunaamini mna uwezo wa kutwaa ubingwa huo,” amesema.

Sambamba na hilo, Waziri Mkuu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa kinara wa maendeleo ya michezo nchini na kuchochea mafanikio yanayoendelea kupatikana katika sekta hiyo.
 
Back
Top Bottom