Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania...
Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako...
Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake...Rais Samia