Rais Samia azindua Kitabu cha Maisha ya Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

Rais Samia azindua Kitabu cha Maisha ya Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi

hivi unaweza kupoteza muda wako kabisa unasoma kitabu cha huyu mzee??unapata faida gani humo ndani?kwa background ip?kwa legacy ipi?
kuna mwingine alikuwa anaitwa mkapa naye alitoa kitabu nasikia,mtanzania yupi??
Sawa we endelea kufatilia maisha ya mondi na zaryyy

Ova
 
Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania...

Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako...

Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake...Rais Samia
 
Mwinyi alifanya makubwa mengi wakati wa awamu yake. Aliipokea Tanzania ya Nyerere ikiwa hoi kiuchumi. Baada ya vita ya Kagera tuliishi maisha fulani ya hovyo sana mpaka 1985.

Mwinyi akawa mtekelezaji wa ERP (Economic Recovert Programs) za Umoja wa Mataifa. Ndipo tukaanza taratibu kuinuka kiuchumi.

Anayeponda huyu mzee kwamba hakufanya lolote inawezekana alikuwa bado anacheza gololi na watoto wenzake miaka ile.
Kujua mambo aliyoyafanya mzee mwinyi inatakiwa uwe na umri pengine miaka 45 na kuendelea, binafsi nina 39 lakini enzi za mwinyi nilikuwa mdogo kiasi ambacho uelewa wa mambo ni mdogo
 
Niliwahi kusikia Mama Sitii alikamatwa Airport Dar akitokea Zenj na dhahabu kibao akiwa safarini kwenda Uarabuni kuziuza. Ikapigwa juu juu na Mrema wa mambo ya ndani. Mzee RUKHSA kwa stories nilizosikia hakuwa msafi hata kidogo.
Hahahahah dili azikwepeki ukiwa jikoni
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Rais wa awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi leo anazindua kitabu kinachohusu maisha yake.

Mgeni rasmi ni Rais wa JMT mh Samia

Tukio litakuwa mubashara kupitia runinga ya Channel ten.

Nitawajuza yanayojiri.

Wahenga karibuni tujikumbushe maisha wakati wa mzee Rukhsa.

Updates;

Mzee Mwimyi ameshaingia ukumbimi na tayari ukumbi umeshasheheni wageni waalikwa mbalimbali.

Sasa anasubiriwa mgeni rasmi Rais Samia.

Rais Samia ameingia ukumbini na sasa wanaimba wiimbo wa taifa.

Ukumbi mzima ni full barakoa.
Uzoefu unaonyesha kwa hapa kwetu viongozi au watu maarufu wakizindua vitabu vya historia ya maisha yao huwa hawadumu hata miaka 2,tumuombee mzee wetu mwinyi aepushwe na balaa hili.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yajayo yanafurahisha ...wastaafu wote wanapewa magari haya ngoja tusubr Bday ya JK sijui na yeye anapewa nini [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847][emoji847]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom