Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Viongozi mbalimbali wameungana na Rais Samia katika uzinduzi huo, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Moustafa Madbouly; Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi; pamoja na viongozi wengine.
JNHPP imeongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini na kuimarisha usalama wa nishati. Kwa sasa, uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini umefikia takribani megawati 4,075, ambapo JNHPP pekee inachangia zaidi ya nusu ya uwezo huo.