Rais Samia azindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo. Asema Serikali imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Tsh 7.35bn hadi 11bn

Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujayo.

Bashe ameomba fedha hizo leo Jumatatu Aprili 4, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.

Bashe amesema bei ya mbolea katika soko la dunia imepanda kwa zaidi asilimia 300.

Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.

Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais fedha hii haitapotea. Tumeshafanya hivi katika korosho kwa kugawa ruzuku ya pembeje na tumeongeza uzalishaji tani 40,000,”amesema.

Aidha, Bashe amesema jumla ya maofisa ugani 7,000 watagawiwa pikipiki na vifaa vya kupimia udongo.

“Tumeanza kuwapa elimu maofisa ugani kulingana ekolojia ya maeneo na mazao yanayozalishwa na tutawapa ekari moja kwa kila ofisa ugani, atapewa mbegu bora na mbolea ili akiwafundisha awapeleke shambani,”amesema.

Amesema kuwa majaribio yameanza katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kwa kutenga mashamba 600 ambapo kila kijiji kitakuwa na shamba darasa ili wakulima wapate elimu stahiki.

Pia amesema maofisa ugani hao watapatiwa vifaa vya kupimia udongo na kwamba hapo mwanzo taarifa za udongo zilikuwa zinapatikana kama za uganga wa kienyeji.

Bashe amesema lengo hadi kufikia mwaka 2025 kila kata iwe na kipimia udongo chake ambapo mkulima atapimiwa udongo na kupewa cheti ambacho kitakuwa na taarifa zote za afya ya udongo wake na aina ya virutubisho vinavyotakiwa.

View attachment 2175655
Hii imekaa poa! Ngoja tuone!!!!
 
Leo maafisa ugani (extension officers) wanakabidhiwa Pikipiki, vipima udongo na simu janja (smart phone) ili viwawezeshe kutekeleza majukumu yao.

Hii fani ya maafisa ugani ilipoteza umuhimu kuanzia miaka ya 1980s. Hongera Samia kwa kumfanya Hussein Bashe kuwa Waziri kamili wa kilimo.
Sometimes kumbe ukiamkaga vizuri unashusha nondo za hatariii na madini yaliyojitosheleza.
 
Mwakyembe alitudanganya kwamba amepata soko la Mchele wa Kyela Marekani , Magazeti yakampamba sana , lakini hadi leo hakuna mkulima aliyewahi kuuza hata debe moja la mchele Marekani.

Unatakiwa uwe kichaa kuwaamini wanaccm
 
Bashe amejitahidi kutoka kwenye ,"Ubunge" na kuuishi uwaziri.

Kuhusu fedha za Kilimo kupitia benki za kibiashara bado nina doubts kama zitawafikia wakulima unless kuwepo na muongozo kamili na dhibiti.
Tungebainisha wakulima strategically na kuwapa mikopo ambayo itarejeshwa yaani tuwe na bodi ya mikopo ya Kilimo.
 
Lengo siyo pesa kuwafikia wakulima moja kwa moja . Fedha ni ruzuku ya mbolea.Mkulima atanunua mbolea kwa bei ya chini.
 
Kile kiwanda cha Dangote vipi? nilifikiri kitatoa nafuu ya bei ya mbolea kwa wakulima wetu
 
Maafisa ugani ni watu muhimu katika kupeleka na kutafsiri matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima, wanasayansi tunapofanya tafiti mara nyingi zinabaki kwenye machapisho ambayo yanaishia kusomwa na watafiti wengine, badala ya mapendekezo kupelekwa kwa maafisa ugani wakawaelimishe wakulima. Wizara ya TAMISEMI inatakiwa kuwa na dawati la kupokea mapendekezo mbalimbali ya watafiti yaliyotokana na tafiti zao ili wazisambaze kwa wagani waliopo halmashauri na kuweza kuwaelimisha wakulima.
 
Hawaamini Hawa Wekeni Akiba Ya Maneno Baada Ya Mwaka Mje Hapa
 
Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujayo.

Bashe ameomba fedha hizo leo Jumatatu Aprili 4, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.

Bashe amesema bei ya mbolea katika soko la dunia imepanda kwa zaidi asilimia 300.

Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.

Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.

“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais fedha hii haitapotea. Tumeshafanya hivi katika korosho kwa kugawa ruzuku ya pembeje na tumeongeza uzalishaji tani 40,000,”amesema.

Aidha, Bashe amesema jumla ya maofisa ugani 7,000 watagawiwa pikipiki na vifaa vya kupimia udongo.

“Tumeanza kuwapa elimu maofisa ugani kulingana ekolojia ya maeneo na mazao yanayozalishwa na tutawapa ekari moja kwa kila ofisa ugani, atapewa mbegu bora na mbolea ili akiwafundisha awapeleke shambani,”amesema.

Amesema kuwa majaribio yameanza katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kwa kutenga mashamba 600 ambapo kila kijiji kitakuwa na shamba darasa ili wakulima wapate elimu stahiki.

Pia amesema maofisa ugani hao watapatiwa vifaa vya kupimia udongo na kwamba hapo mwanzo taarifa za udongo zilikuwa zinapatikana kama za uganga wa kienyeji.

Bashe amesema lengo hadi kufikia mwaka 2025 kila kata iwe na kipimia udongo chake ambapo mkulima atapimiwa udongo na kupewa cheti ambacho kitakuwa na taarifa zote za afya ya udongo wake na aina ya virutubisho vinavyotakiwa.

View attachment 2175655
Ni kamarada H.Bashe tena....

Bashe anaweza....

Bashe is a visionary leader....
Bashe is a charismatic leader.....

TUNATEGEMEA mengi kutoka kwake ,amin🙏

#Siempre JMT🙏
 
😍
 
Bashe amejitahidi kutoka kwenye ,"Ubunge" na kuuishi uwaziri.

Kuhusu fedha za Kilimo kupitia benki za kibiashara bado nina doubts kama zitawafikia wakulima unless kuwepo na muongozo kamili na dhibiti.
Tungebainisha wakulima strategically na kuwapa mikopo ambayo itarejeshwa yaani tuwe na bodi ya mikopo ya Kilimo.
Hizo 150 billions haina maana watawapa wakulima, zitatumika kama security ili wakulima waweze kukopa kwenye hizo commercial bank, maana kwa sasa Bank nyingi hazitoi mikopo kwa wakulima maana ni high risk business na wamepoteza pesa nyingi sana
 
Back
Top Bottom