Rais Samia azipeleka juu Mbaazi, Choroko, Dengu, Ufuta, Alizeti, Kahawa, Karafuu. Kwani wakulima wao wanasemaje?

Kanda ya ziwa pamba imenunuliwa kwa tsh. 1750, toka tsh. 900 ya mwaka jana. Bahati mbaya wengi hawakulima mwaka jana baada ya kuchoshwa na Bei,mkopo na mvua kubwa zilizopitiliza na ugonjwa wa pamba kuzeeka ( kuwa nyekundu) kabla ya wakati.
Km wakulima wengi hawakulima mwaka jana means Supply imekua ndogo then Demand imekua kubwa, which means price lazima ipande kwakua wanunuzi wapo teyari kulipa bei ya juu kunyang'anyana kidogo kilichopo..
supply is inversely proportional to demand.

Na hiki ndicho kilichotokea ht huko duniani, watu walijifungia hawakulima or Kuzalisha wametumia akiba imeisha now wanatafta malighafi kwa bei yoyote...

Na hili limejitokea ht kwa mafuta ya kula kupanda kutoka 3000 kwa Lita mpaka 8000 kwa Lita, or Mbolea kupanda bei...
ila wapiga matarumbeta hawatafuti majibu ya kitaalam wanakuja na mapambio.

Sasa subirini dunia ikawe sawa na covid. wazalishaji wakubwa huko america ya kusini warudi mashambani then tutarudi kuujadili huu uzi.
 
Yeye anazinunulia wapi huyo Raisi nimpelekee
 
Mleta mada ndio Musiba wa awamu hii
 
Wanasema Asante Covid 19 kwa kuwachapa kwa hakika wahindi mpaka jeuri ya rais wao Modi kuwasupport kulima mbaazi,choroko nk,zikalegea na kshindwa maana walaji wakui ni wahindi.
Shukrani za pili kwa uchina Kama kweli walitengeneza hiki kirusi rafiki kwa bara la afrika
 
Hapo kupungua kwa wakaanga mihogo nimecheka sana.
 
Hizi sifa nyingine zinalenga kumharibia na sio kumjenga. Mwakani bei itakaposhuka napo mtamlaumu?

Amandla...
 
Kwani kampeni zimeshaanza? Wengine nao wakianza kampeni zao msiwapeleke kwenye kamati.
Nilikuwa najiuliza hili bandiko na komenti mbona zimekaa kishabiki shabiki, but jibu ndilo hilo aseee😃!.
 
mkuu hivi biashara ya mazao inalipa?
 
Mimi nimepiga ela choroko ufuta na mbazi sasa tunasubiri korosho na pembejeo tumepokea mara mbili bure,hiv mama alichelewa wapi,raha sana!! ila afanyefanye atupe katiba mpya.
 
Mahindi na mchele vitazame kwa jicho la tatu mama, wasukuma tuna mda mrefu hatujaongeza mke.
 
Kusema ukweli mama ameweka mazingira mazuri ya biashara ya mazao baada ya kuboresha mahusiani na majirani na jumuia ya kimataifa na pia kuondoa yale ma non-triff barriers. Mama Samia kwenye hili amejitahidi sana. Anasitahili pongezi na kutambuliwa. Mazao yote kwa sasa bei ziko vizuri sana.
 
Mbona mimi niko Bukoba na simtaki 2025? Ongelea nafsi yako sio unajumuisha wengine.
Uko bukoba ya wapi mkuu?

Wananchi wengi wa Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla wanamkubali sana mama.

Labda wewe ni wale polisi au tra waliokatazwa kutumia mabavu na kinambikia watu makesi kwa hiyo umekosa ulaji...polee...utazoea tu mdogomdogo.
 
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mwakajana nilinunua ufuta 1500 nikauza 1300 hasara,nikanunua mbazi 450 kika uza 250 hasara.mwaka huu tumepiga pesa,na korosho sijui itakuwaje,kwamara ya kwanza kusini pembejeo tumepewa bure!sisi tunamuombea dua mzuri MAMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…