Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Hongera kwa kanisa....nimesikia kituo kikubwa kinajengwa Bagamoyo...Kiromo....kilichopo Dar ni kidogo...hongera kanisa.....Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025.
Rais Dkt. Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya afya ya akili. Viongozi hao wa Kanisa wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa kwa Kanisa hilo.
Aidha, kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya akili, Serikali imeahidi kushirikiana na Kanisa ili kujenga Kituo kikubwa zaidi ili watoto wengi waweze kupata huduma hiyo.
Aiseee!Ni kawaida kwa kiongozi wa serikali mwenye wananchi wengi waliomwezesha kupata kura kukutana na viongozi wa dini wenye waumini wengi nchi nzima
Sababu hao viongozi wa dini zenye waumini wengi ni wawakilishi wao kuliko hata wabunge na huenda na solution sio kelele
Raisi hawezi kutana na mtu kama Askofu Mwamakula ambaye hata kanisa analosalisha Dar hakuna ajuaye
Hao wanaachiwa akina Lisu ndio wazurure naye.Waumini hana kakofia na nguo ya askofu kajishonea mwenyewe nyumbani kwake na cherehani yake
KKKT isihoji mambo ya uchaguzi.Wamezungumza nini?
Ili waokoe jahazi bila mafanikioKina malasusa?
achaga ujinga basi!Kila mtu na shida zake na jitihada zake Mungu ni wetu sote nitahangaika na yangu tu ya wengine pesa mbele hutaki acha ufala mwisho kitonga
Njaa mbaya sanaHii ndio hali halisi, unaweza kuambiwa lolote lakini wewe mwenyewe jiongeze
================
Rais Samia Suluhu amefanya mazungumzo na uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya afya ya akili, ambapo Serikali imeahidi kushirikiana na kanisa kujenga kituo kikubwa
View attachment 3300968
Ujinga ni upumbavu wa akili zako mwenye shobo, usinifate fate pita kushotoachaga ujinga basi!