Rais Samia azungumza na Wananchi Kilangalala Mkoani Geita, Leo Oktoba 15, 2022

Rais Samia azungumza na Wananchi Kilangalala Mkoani Geita, Leo Oktoba 15, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan azungumza na wananchi Kilangalala Mkoani Geita leo tarehe 15 Oktoba, 2022 ambapo pia alitembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Chato na kuzindua Kituo cha Kupoozea Umeme na Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu mkoani humo.

=====
  • Rais alianza kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Chato, Geita akiwahakikishia wananchi hospitali hiyo itamaliziwa kujengwa kama ilivyokusudiwa, akiwasisitiza wananchi kujiunga na bima ya afya mfumo wa bima ya afya kwa wote utakapokuwa tayari.
  • Rais Samia alifika Buseresere Katoro, Geita ambapo aliahidi kutatua changamoto za wananchi na kuwaasa wafanye kazi kwa bidii.
  • Rais Samia alifika kuzindua Kituo cha Kupooze umeme cha Mpomvu, Geita.
  • Rais Samia amefika na kuzindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Geita.

Kilangala Geita
Waziri wa Nishati - January Makamba

  • Kabla ya mwaka 2025 umeme utakuwa umefika katika kila kijiji mkoa wa Geita.
  • Serikali imetenga bilioni 57 kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo kuondoa adha wanayoipata ya kutumia majenereta kwenye shughuli zao.
  • Serikali imetilia mkazo zaidi kwenye gridi ya Magharibi inayojitegemea kuzalisha umeme mwingi zaidi kutokana na matumizi ya eneo hilo kuwa makubwa.
  • Mkoa wa Geita kuwa kati ya mikoa itakayopewa kipaumbele kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa yanayoua akina mama na watoto wengi nchini.

Waziri wa Afya - Ummy Mwalimu
  • Serikali kuhakikisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya kanda Geita unafanyika, ambapo huduma zote za kubwa na ubingwa bobezi zitatolewa kama vile magonjwa ya moyo, saratani na magonjwa ya ndani.
  • Ujenzi wa jengo la mama na mtoto Chato kuanza ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/2023.
  • Wananchi waendelee kuchukua tahadhari kutokana na ugonjwa wa Ebola, Kipindupindu na Uviko-19 kwa kuzingatia kanuni za usafi binafsi na usafi wa afya ili kuepukana na magonjwa hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - Angellah Kairuki
  • Kupitia fedha za Uviko kuanzia Januari 2023 magari ya wagonjwa takribani 368 kuanza kugaiwa kwa kila halmashauri, na kila mkoa gari moja moja kwa uratibu wa afya nchi nzima.
  • Watumishi ambao badala ya kulala Nzera wanatumia magari ya umma kuwatoa sehemu nyingine kwenda Nzera kuacha tabia hiyo mara moja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Samia Suluhu Hassan

  • Geita inaenda kupata umeme wa kutosha na uhakika wa Megawat 90 kuendesha shughuli zake ambapo itasaidia pia kuvutia wawekezaji.
  • Watanzania wadumishe amani, utulivu, umoja na mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ili kuzalisha zaidi na kuleta maendeleo.
  • Kufanya ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha shughuli za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara za madini zinafanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta ya madini.
  • Kutoa elimu juu ya sheria za madini kwa wadau mbalimbali kupitia mafunzo maalum. lakini pia kushirikiana na idara nyingine za serikali na vyombo vya dola kusimamia biashara ya madini na kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini.
  • Kuwaunganisha wachimbaji wadogo na taasisi ya jiolojia ili kuongeza tija kwenye shughuli za madini.
  • Kodi kwa wenye viwanda vya madini ziangaliwe ili kuleta tija kwenye biashara hiyo.
  • Ujenzi wa barabara kutoka Kakola kwenda Kahama kuanza karibuni.
  • Geita kuwa kitovu cha ukuaji wa uchumi ndani ya taifa na ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo wananchi kutumia fursa hiyo vizuri kubadili mfumo wa kiuchumi.
  • Ahadi ya milioni kumi kwa kila mkoa kujenga ofisi za machinga, fedha hizo zipo tayari, TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa kusimamia jambo hilo kuhakikisha jambo hilo linafanyiwa kazi. Lakini pia kuhakikisha wamachinga watapewa bure maeneo kujenga ofisi zao, maeneo ambayo yatakuwa karibu na sehemu zao za kazi na si vichochoroni.

Safi Sana mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania ambaye muda wote na wakati wote yupo kazini kuwatumikia watanzania na kuwasikiliza kero zao na mwisho kutoa majibu ya utatuzi wa kero zao, hakika Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia kuwa Nayo hapa nchini
 
Wote ni lazima waende kwa Kagame, hata Ruto yuko huko, Kagame ndiyo Big Boss!
 
Niseme tu Rais tangu aingie madarakani amekuzuru kanda ya ziwa zaidi ya mara tatu au nne ili hali kuna kanda hajatia mguu,sababu mnaijua?niseme nisiseme?je ziara zake zitasaidia hicho anachokiplania
 
Waha kesho Mh.Rais anakuja kwenu Kg mpokeeni kwa shangwe ale Ntore kwa wingi sana.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzungumza na wananchi Kilangalala Mkoani Geita leo tarehe 15 Oktoba, 2022

=====
  • Rais alianza kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Chato, Geita akiwahakikishia wananchi hospitali hiyo itamaliziwa kujengwa kama ilivyokusudiwa, akiwasisitiza wananchi kujiunga na bima ya afya mfumo wa bima ya afya kwa wote utakapokuwa tayari
  • Rais Samia alifika Buseresere Katoro, Geita ambapo aliahidi kutatua changamoto za wananchi na kuwaasa wafanye kazi kwa bidii.
  • Rais Samia alifika kuzindua Kituo cha Kupooze umeme cha Mpomvu, Geita.
  • Rais Samia amefika na kuzindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Geita.

Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo nchini hana muda wa kupumzika kazi kazi kila siku
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzungumza na wananchi Kilangalala Mkoani Geita leo tarehe 15 Oktoba, 2022

=====
  • Rais alianza kutembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Chato, Geita akiwahakikishia wananchi hospitali hiyo itamaliziwa kujengwa kama ilivyokusudiwa, akiwasisitiza wananchi kujiunga na bima ya afya mfumo wa bima ya afya kwa wote utakapokuwa tayari
  • Rais Samia alifika Buseresere Katoro, Geita ambapo aliahidi kutatua changamoto za wananchi na kuwaasa wafanye kazi kwa bidii.
  • Rais Samia alifika kuzindua Kituo cha Kupooze umeme cha Mpomvu, Geita.
  • Rais Samia amefika na kuzindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Geita.

Mkuu acha upotoshaji, rais hataongea na wananchi bali atawahutubia. Viongozi wanaongia madarakani kwa kunajisi box la kura huwa hawaongei na wananchi, bali huwa wanawahutubia.
 
Kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Samia Suluhu 2025 hana mpinzani
 
Barabara ya kahama -Kakola hadi geita tulisubiri kwa muda sana.
 
Back
Top Bottom