Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa/ Vikosi katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, leo tarehe 30 Agosti, 2022
==
Samia Suluhu Hassan amesema anazo taarifa kuwa baadhi ya maofisa wa polisi kutumia mafuta yanayotolewa na Serikali katika kuendeshea magari yao binafsi yasiyo na uhusiano na kazi za kipolisi. Rais amesema anao ushahidi wa majina ya wahusika pamoja na namba za magari hayo.
Aidha, amelitaka jeshi la polisi kuongeza matumizi ya tehama katika kufanya kazi zake, kuboresha kitengo cha mawasiliano ya ndani na yale yanayohusisha viongozi wakuu wa nchi pamoja na kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo yamekuwa yanaripotiwa kila mwaka.
Amemtaka CAG kuendelea na kazi nzuri ya ukaguzi anayoifanya pamoja na kumsisitiza aendelee kufichua uovu wa matumizi mabaya ya pesa ndani ya taasisi hii.
Katika kuhakikisha haki inakuwepo, Rais amewataka polisi kuacha tabia ya kubambikia watu kesi pamoja na kuwaweka ndani pasipo kuwa na ushahidi, au ushahidi huo kutokuwa umekamilika. Jambo hili linatia doa taasisi hii pamoja na kuiongezea bajeti Serikali katika kuwatunza mahabusu hawa. Rais amezungumza haya kwa kurejea takwimu za watu walioachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi ambao idadi yao imefikia watu 1840.