Rais Samia: Baadhi ya maafisa wa Polisi huiba mafuta ya Serikali kuendeshea vyombo vyao binafsi

Dawa ni kwa serikali kurudisha allowance kwenye mishahara ili watumishi waweze kugharimia usafiri wa kwenda na kurudi makazini, huenda hao polisi kwenye hiyo mizunguko na magari yao huenda bado wanakuwa wanatekeleza majukumu yao ya kikazi, maana wakati mwingine inakuwa ngumu kujua ni wakati gani polisi yupo kazini au hayuko kazini, labda kama awe amestaafu kazi, ni mtazamo tu lakini.
 
Bila shaka wewe ni polisi, wasilisha hoja yako kunako husika!
Acha Uganga wa kienyeji, hii ni mada iliyoletwa tujadili, pls elekeza maoni kwenye mada, mimi nipo Safi kabisa na ninakula pensheni huku lingusenguse, Ruvuma
 
Acha Uganga wa kienyeji, hii ni mada iliyoletwa tujadili, pls elekeza maoni kwenye mada, mimi nipo Safi kabisa na ninakula pensheni huku lingusenguse, Ruvuma
Kwani ukiwa polisi ni dhambi au unakuwa mchafu na pensheni huwezi kula?
 
Rais asiwaonee tuu mapolisi bali maofisa karibu wote wenye magari ya serikali wanafanya hivyo..

Tatueni hili Kwa kuweka utaratibu mzuri wa matumizi ya mafuta..
 
Kuna wengine nawaona hapa wanamwagilia moyo hapa na Noah yao nahisi ni mafuta ya tozo wanatumia[emoji23][emoji23] kuwakimbiza Wanyantuzu hapa
 
Mi kuna siku boda boda yangu ilikamatwa ilapelekqa kituoni basi dereva akanipigia mi nikatoroka ofsin chapu nikaenda kuta imefungiwa kule msimbazi nyuma kabisa na chain juu basi nikamwita yule dogo akanionyesha askar aliemkamata nikamhoji baada ya hapo dogo akaniambia boda ilikuwa na mafuta full tank kuangalia tyre ya mbele imshabadilishwa na mafuta wameyatoa na side mirow zimefunguliwa na starter imebadilishwa basi pale nikaanza na kazi ingine ya kulipwa maana dogo alivyoipeleka walipomuamuru aliipiga picha ushahidi ukambana tule askari mbona aliniita pembeni tukaelewana maana kama alinishtukia fulani naweza muharibia kibarua
 
Geshi la borish taabu tupu.

Wale jamaa lawama ni yingi mno.

Kabla ya kulivunja inahitajika maombi ya deliverance maana ni kama wana laana flani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…