Rais Samia, Bado hujaona hili ni tatizo tu?

Chanzo cha Kelele ya Corona ni hawa hawa watu mandumila kuwili...mimi nikimuona yule mama eti ni Waziri wa Afya nashangaa sana...Unafiki umewajaa...nani atawaamini...
 
Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu.

Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.

Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mtano. Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.

Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo,

Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.

Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo.

Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendelea kuwepo.

Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?

Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika.

Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

View attachment 1868346
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji106][emoji106]
 
Ni kweli kabisa, alifanya kosa la kiufundi kutovunja serikali aunde yake. Wengi tulitarajia hilo. Alidhani urais alioupata alipewa fadhila ilhali alipigiwa kura na alipiga kampeni sana nchi nzima kuliko hata magufuli.

kwa kadri ambavyo anamuona Mbowe na Chadema ni tishio kwake ndiyo ambavyo hawa vijana wakabila na wadini walikubuhu watakavyoendelea kumtia vidole vya macho.

Na hajashtuka kwamba kuendelea kuwashambulia wapinzani anadhani polisi wanamsaidia, somebody tell her that it is a subotage. Chuki kubwa inaanza kujengeka katika jamii dhidi yake.

Na sasa amekaa kimya polisi kustorm kanisani, jambo ambalo hata jpm hakuwahi kuruhusu likafanyika ijapokuwa aliwaharass sana wapinzani.

Time is a good judge
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kosa Kubwa Ni vile Mama alicopy wale wale watu ambao waliumiza sana Wananchi wenzao...wengine anawajua kwa karibu zaidi hivi kweli Mh Rais Hujui Ubaya wa Joseph Malongo??? Hujui mabaya aliyotenda pale ofisini kwako??? Hujui uzushi aliozushia watumishi pale huku akitamba wazi yuko karibu na Mh Magufuli?? Na akisema yeye ni seniour. yeye ni mmoja tu wa watesi wengi waliotesa watu ofisi ya VP yote inajua ubaya wa Malongo na genge lake alilojenga na bado yuko serikalini. Sio yeye tu na wengine wengi wapo na wameumiza sana watu..Kuna kesi zilifunguliwa za ajabu ajabu waliofanya hayo wapo serikalini..Mama hawa watakusumbua na wanataka ukwame ..fukuza hawa anza na watu wako...

LAKINI BADO yuko Serikalini...Ungeunda Serikali yako hawa watakuchanganyia madesa..fukuza hawa watu.
Uhuru wa kutoa maoni usiutumie kama uhuru wa kusambaza majungu na upotoshaji. Jamii kama ni nyingi mnafanya kundi fulani hapa nchini likipata madhara, watu wanakaa kimya bila kupata sauti.
 
Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu.

Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.

Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mtano. Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.

Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo,

Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.

Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo.

Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendelea kuwepo.

Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?

Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika.

Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

View attachment 1868346
Umezunguka sana yeriko usimuingize mtumishi wa Mungu kwenye ugaidi wenu, li mbowe ni ligaidi, kama unachanja chanja na familia yako wengine tumestuka. Muda ni mwalimu mzuri, tafuteni utetezi wa kumsaidia gaidi sio kumshambulia mpakwa mafuta wa Bwana. Sio bure unatafuta uteuzi
 
inawezekana anawaogopa sukuma gang...laiti angenipa urais kwa masaa sita tu ndipo wangejua kwa nini utingo ni mtu muhimu sana wakati wa safari
Yaani wewe uraisi Mimi angenipa ukuu wa huko alipo huyo mbwabwajaji tu ningemsaidia kumuelewesha kuwa Watanzania tunajitambua na Mama tumemuelewa
 
Hestancy ya wananchi walio wengi kuchanjwa Chanjo ya Corona inaonyesha jinsi wananchi walio wengi walivyokua wanamkubali JPM. Itachukua miaka mingi Sana kwa Fikra na mitazamo ya JPM kufa miongoni mwa raia. So far majority ya wafanyakazi wa sekta ya afya ambao tulitegemea watoe elimu ya Chanjo hawako tayari kuchanjwa. Kimsingi waliopitisha Chanjo imekula kwao, sisi tuko na Bishop Gwajima.
 
Kwan Samia yeye ni nani kwamba hawezi kupewa rushwa? Ukweli pamoja na kwamba kuna changamoto ya corona duniani kote ila pia suala hili ni biashara Kwa watu wengine na wanatengeza hela kubwa sana, usalama wa taifa wa nchi hii pia na wao siku hizi wamekuwa na maslahi yao kwanza ndo maana unaona kuna vitu vinafanyika mpaka unajiuliza kwamba nchii kuna usalama kweli ???
 
Tat
Adui mkubwa katika serikali ya huyu mama ni Hawa dizaini ya watu Kama Nchemba,Gwajima na wengineo, sio hao wapinzani wapiga kelele tu hawana madhara, mama akicheka na Hawa Sukuma Gang watamkwamisha kweli, wao akili na malengo yao Ni mwaka 2025 Urais waweke mtu wao

Hilo genge limejaaa serikalini hata Makatibu wakuu wamo...Mama Anatakiwa alitambue hilo Genge alivunje alitoe..Asipofanya hivyo atashangaa..
 
Ni kweli kabisa, alifanya kosa la kiufundi kutovunja serikali aunde yake. Wengi tulitarajia hilo. Alidhani urais alioupata alipewa fadhila ilhali alipigiwa kura na alipiga kampeni sana nchi nzima kuliko hata magufuli.

kwa kadri ambavyo anamuona Mbowe na Chadema ni tishio kwake ndiyo ambavyo hawa vijana wakabila na wadini walikubuhu watakavyoendelea kumtia vidole vya macho.

Na hajashtuka kwamba kuendelea kuwashambulia wapinzani anadhani polisi wanamsaidia, somebody tell her that it is a subotage. Chuki kubwa inaanza kujengeka katika jamii dhidi yake.

Na sasa amekaa kimya polisi kustorm kanisani, jambo ambalo hata jpm hakuwahi kuruhusu likafanyika ijapokuwa aliwaharass sana wapinzani.

Time is a good judge
Naona mnaupiga mwingi mpaka mpira unatoka nje na adui ndio anaenda kurusha mpira
 
Gwajima ni katika Kundi kubwa la Wasukuma wanao a mini katika Mfumo dume kama walivo wamasai
Hongera zako kwa kuamini mfumo jike mimi siyo msukuma ila mfumo dume ndiyo mfumo sahihi wa kufuata
 
Usemacho ni kweli mtu kawekwa Kati,ukiacha hao wengine nilimsikia Karibu mkuu wizara ya Afya akiongelea hatua za kuchukua ila kwenye chanjo aliongea as if sio kitu cha muhimu .

Nadhani Rais hajachelewa Sana Felix Chisekedi alivunja Ushawishi wa Kabila baada ya miaka 2 ,Mama arudi haraka kwa JK amsaidie kusuka system yake kuanzia kwenye usalama,ndani ya chama,Serikalini afu kwa Wananchi kutaji set kwenyewe.
Kwenye chama subiri uchaguzi wa mwakani ndani ya Ccm ndyo tutajua rangi halisi ya mzenji
 
Back
Top Bottom