Rais Samia, Bado hujaona hili ni tatizo tu?

Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu.

Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.

Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mtano. Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.

Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo,

Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.

Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo.

Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendelea kuwepo.

Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?

Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika.

Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

View attachment 1868346
Ndugu yangu Yeriko, ukiweka kando ukada, unaandika vitu vya msingi sana. Kongole kwa bandiko hili 👌
 
Tukiwa wakwel kabisa tukaacha unafiki, tukaacha kuogopana na kutishana, chanjo si suluhisho, na Wala haitakuwa suluhisho, there is hidden agenda ahead/btn.
 
Huyo Chisekedi ni bure kabisa hafai kuwa wa kfano.
Ameendeleza hila la Kabila kwa wapinzani wa kweli wa Kabila.
Ametunga mswada wa sheria ya kuzuia raia wa nchi yake ambaye mzazi wake mmoja siyo raia wa Kongo lengo likiwa kumzuia Moise Katumbi asigombee uraisi uchaguzi ujao.

Watanzania tutafute taarifa na maarifa kabla ya kushabikia watu na mambo yao.
Ni sawa ulitaka amruhusu Ili iwaje? Rwanda waendelee kula mali ya DR Congo?
 
Gwajima katwambia kuwa kundi moja lililopendekezwa kuchanjwa kwa lazima ni Majeshi, japo naamini kasema hayo kwa nia njema, Jamaa kawapa hint vyombo vya ulinzi na Usalama kuwa Chanjo haifai, Sasa kama huku siyo kutengeneza mazingira majeshi kuigomea serikali ni nini?
Hhh' haaaa!

Ulichokiandika ni kweli.
 
Ayubu alikua spika wa redio Chato, anajua siri nyingi za ndani na ndiyo anapata kiburi cha kumuonyesha madam kuwa hambabaishi.
Hao wabunge wote aliowaingiza Magufuli ndani ya Bunge, naAyubu mwenyewe, leo hii Samia Mwenyekiti akisimama na kuwaamuru wamtupilie mbali huyo kikaragosi wa Mwendazake hazipiti dakika tano Ayubu ananywea kwa aibu.

Hakuna mbunge hata mmoja atakayepinga kumwondoa spika wakati wowote ndani ya bunge lile.
 
Bora hata VP,PM mwenyewe ni kama kaisusa Serikali...mama fukuza Hawa watu kwanza imefika mahala hata makusanyo ya serikali hawashughuliki kuhimiza kama mwanzo,watu wanaiba dawa za serikali hazifiki za kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma nk ..Sasa Wana msaada gani hawa
Hivi PM alisha teuliwa upya au anaendelea na kiapo cha awali?
 
Bora hata VP,PM mwenyewe ni kama kaisusa Serikali...mama fukuza Hawa watu kwanza imefika mahala hata makusanyo ya serikali hawashughuliki kuhimiza kama mwanzo,watu wanaiba dawa za serikali hazifiki za kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma nk ..Sasa Wana msaada gani hawa
Msitafute wachawi. Kama mama anarembulia walipa kodi na kuwchia watu wafanye watakavyo asubiri maumivu maana mziki bado
 
Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu.

Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.

Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mtano. Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.

Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo,

Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.

Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo.

Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendelea kuwepo.

Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?

Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika.

Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

View attachment 1868346
Umeandika utumbo kaka.!
 
Ww mpuuzi kama walivyowapuuzi wengine! Serikali ya awamu ya 5 unayoiita ya udharimu huyo mama yako hakuwemo? Acha ujinga wa kuweka kabali/wedge, hutafanikiwa!
Mungu ibariki Tz!
Acha unafiki Mungu hawezi ibariki nchi yenye wajingawengi kama wewe
 
Tatizo ccm wamechanganya siasa na corona na hii mijitu kamwe haiaminiki,
 
Back
Top Bottom