Rais Samia: Bado ninaisikia sauti ya Hayati Magufuli akiniambia kuhusu miradi na Dodoma kuwa Makao Makuu

Shukrani kwa ufafanuzi mzuri!Maana yake kama gari inatoka Dar kwenda singida,ikifika mtumba inaweza kuchepuka.Kwahiyo inaweza ikachepukia either kaskazini au kusini (kwa maana pande zote zitakuwa zinatoa?)au itakuwa inachepuka upande mmoja tuu...Pia kama unajua naomba nielekezee barabara hizo au hiyo ya mchepuko itapita mitaa gani kabla ya kutokeaa hapo Nara.
 
Ni suala la msingi amalize miradi ya mtangulizi wake kama hayati alivyofanya kwa Jakaya. Ingawa ameonyesha uwezo zaidi pia kwa kuanzisha ya kwake. Hongera Mama Samia.
Mwendazake aliendeleza mradi wa gesi na bandari ya bagamoyo? SGR ilikuwa iende Kigoma...
 
inayoelekea kusini inapita ihumwa
kwenda hadi iyumbu
alafu inaelekea magharibi kuitafuta nara,
huku kaskazin inakatiza mji wa kiselikari
inatokezea mahoma makulu
inaendelea hadi nzasa
kisha makutupora
alafu inaitafuta nara
bila shaka wewe ni
mnyausi
maana hilo jina la kukaya,
 
Duuuh kuu street ni finyu mkuu??
 
Ok asante sana wa kukaya
 
Mama anaendelea kutekeleza mipango ya hayati Magufuli ya kulifanya jiji la dodoma kuwa na miundombinu bora kabisa.
Mipango sio matumizi, marehemu hawezi kufufuka mnapoteza mda,signature na alama itabakia kuwa ya Samia..

Habari za sijui alianzisha sijui nini,mipango na vya kuanzisha viko toka enzi za Mwalimu.
 
Kuna baadhi ya watanzania, wanaroho za ajabu na ubaguzi, Dodoma ni sehemu ya Tanzania, hivi kinachomuuma mtu kuisema sehemu ya Tanzania vibaya ni nini? Unaposema Dodoma ni mbaya ulitaka iweje? Unakosoa uumbaji wa Mungu ktk dunia? Unadhani maeneo yote yakifanana tutaenda kufanya utalii wapi? Tunahitaji utofauti ili kuwe na hali ya kushangaa maeneo mengine na kuyatembelea.

Wanadamu tumepewa mahalifa na Mwenyezi Mungu, hivyo Dodoma bado itapendezeshwa tu. Kama Dubai ilivyokuwa na uasili wake wa jangwa lakini sasa inamaeneo yenye uoto wa mimea. Swala la barabara finyu katikati ya mji ndo staili na design ya mji huo. Unataka katikati ya mji kuwe na barabara pana, kwani unapitisha nini zaidi? Ndo maana barabara pana na kubwa zinapita kando ya mji.

Tutajie ambapo wewe unaona palifaa kuwa makao makuu. Make ukileta ukosoaji, tunauwezo wakukosoa hata wewe kule unakodhani panafaa. Hakuna sehemu iliyokamili. Tuache ushamba. Miji yote inauzuri na utofauti wake unaoifanya iwe ya kipekee.
Ati unaanza tu kukashifu mkoa kuwa ni mbaya, hivi wewe ndo mtaalamu wa kujua upi mji mzuri na upi mbaya. Ebu tutajie mji wewe unao ona ni mzuri, nasi tukuoneshe uwazacho sicho.

Penda nchi yako, penda Taifa lako, jivunie kilichopo kwenye nchi yako, Dodoma ni sehemu ya Tanzania. Na ni makao makuu. Makao makuu hayachaguliwi kwa kufuata ukubwa wa mji au sijui huo uzuri unao sema! Ha ha ha!
 
Mizimu ya chato iko imara
 
Porojo tu hizo. Magufuli ndio alimwambia atukimbize wamachinga mpaka tunajuta kuzaliwa?
Teh teh teh...πŸ˜‚πŸ˜‚... unazingua man..teh teh πŸ˜‚
 
porojo tu
mbona hukusikia akikuambia kuhusu polepole , ndugai na Lukuvi ?
 
Kabisa mkuu yaani huyu mwamba angeongezea hata miaka mitatu mbele nchi hii tungekuwa nusu ya South japo yeye alienda mbali zaidi eti kama Europe [emoji4]
Tatizo gaidi asingekuwa ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…