Tunaweza kubadilisha mwngi kuifanya Dodoma inawiri lakini itaendelea kuwa mbaya kwa sababu ubaya wa Dodoma ni wa asili. Hali ya hewa ni mbaya, hatuwezi kubadilisha. Ardhi yake ni mbaya, tunaweza kurekebisha kiasi lakini hatuwezi kubadilisha.
Lakini pia hata yale ambayo hufanywa na mwanadamu, Dodoma yamefanyika hovyo sana. Dodoma ina barabara finyu katikati ya mji. Yaani Tabora iliyopangwa na wajerumani mwishoni mwa miaka ya 1800, ina barabara pana na ina mpangilio mzuri maradufu ya Dodoma iliyopangwa na CDA miaka ya 1980, yaani Wajerumani wa miaka ya 1800 walikuwa na akili na weledi kuliko wataalam wa CDA wa miaka ya 1980.