Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 7,225
- 9,830
View: https://youtu.be/auju_W7Vb7s?si=Wuj4m10xKf-8OHSX
Kama Raia Mzalendo ninaye ipenda nchi yangu, kwa heshima na taadhima naomba nimshauri Mama yetu, Rais wetu na Shangazi yetu anaye upiga mwingi, akae chini na atafakari kinachoendelea ndani ya Utawala wake kwa sasa kuelekea GE-2025.
Hali inatisha, inaogopesha na ina hatarisha UTAWALA BORA, AMANI na HAKI ya nchi yetu, DEMOKRASIA na UHURU tulio upata miaka zaidii ya 60 ilopita.
Mwaka huu unaweza kuwa mbaya sana ktk historia ya nchi yetu Tanzania iwapo Rais SSH hatochukua hatua madhubutu, za dhati na za utashi wa kisiasa ili kunusuru Taifa lisiingie kwene umwagazi wa damu usio wa lazima kama ilivotokea Januari, 2001 kule Zanzibar.
Kinachotakiwa sasa bila kuchelewa, ni Rais Samia kuitisha kikao cha dharura kitakacho wakutanisha wafuatao:
1. Viongozi Waandamizi CHADEMA.
2. Viongozi Waandamizi CCM.
3. Viongozi Waandamizi INEC.
4. Viongozi Waandamizi TLS.
5. Viongozi Waandamizi wa DINI mbalimbali.
6. WAZEE WENYE BUSARA: MZEE WARIOBA na MZEE BUTIKU.
Kwa hapa tulipofikia na matukio ya kutisha yanayo endelea kujitokeza na kuhatarisha Haki, Amani, Uhuru na Demokrasia ya nchi yetu ni lazima yashughulikiwe.
Naomba kuwasilisha.