Rais Samia: Demokrasia ni kuheshimu Sheria, heshima ya Mtu inakuja kwa kuheshimu Sheria za Nchi, ombi la Zitto kuhusu kesi ya Mbowe lajibiwa

TZ kama shule tu, wanafunzi wachache ndio wanaweza kujenga hoja dhidi ya mkuu wa shule, wengi ni vinabo mafalatee
 
Sheria zipo zilishatungwa, tunapaswa kuishi kwa kuzifuata zinavyotuelekeza..kwenda kinyume chake ni kutozifuata au kuzitii...matokeo ya kutozifuata na kuzitii ni kupambana na vyombo vya dola..

Mfano: Kama sheria inasema kuandamana lazima upewe kibali cha polisi, ukiandamana bila kibali utakuwa umeivunja, kama sheria inasema kukutana na kufanya mkutano wa hadhara lazima uwe na kibali kutoka kwa mamlaka na wewe ukafanya bila kibali utakuwa pia umevunja sheria....
 
Rais ambaye ni mshitaki/mlalamikaji ili mahakama ihukumu (watumishi wa uma akiwepo DPP wanafanya kazi zao kwa mapenzi ya Rais), anaweza kuondoa malalamiko/mashitaka yake wakati wowote.
Hata hivyo, anaruhusiwa kisheria na kikatiba kusamehe hukumu zilizotolewa mahakamani, ambapo kwa Mbowe bado.
 
Kuna maswali muhimu ya kujiuliza
Afuate sheria gani? Kavunja sheria gani?
Amheshimu nani? Ni nani kamkosea heshima?
Kwahiyo kesi yake sio ugaidi tena? Bali ni maswala ya sheria na heshima?
Kufuata sheria ni kutovunja sheria. Hivyo kama ameshitakiwa kwa ugaidi, maana yake kavunja sheria ya ugaidi. Na ndiyo maana kesi hiko mahakamani ili mahakama itoe uamuzi. Kuvunja sheria ni kosa.

Nashangaa unapouliza kavunja sheria gani wakati tayari ameshitakiwa kwa sheria alovunja kuhusu ugaidi na yupo mahakamani.
Swala la heshima pamoja na kufuata sheria za nchi, ni vizuri kuheshimu mamlaka za nchi. Ukisoma katika mashitaka yake alifanya njama za kutaka kuhatarisha maisha ya kiongozi alotajwa. Heshima ni muhimu, usipokuwa na heshima unaweza pata wazo la kuondoa uhai wa mtu.

Mama hajasema kesi yake si ya ugaidi. Fahamu kwamba ugaidi ni kuvunja sheria za nchi. Na unapofikia kutokuwa na heshima basi hii itakufanya utende kosa kwani utasukumwa na mihemko ambayo utafanya maamuzi mabaya kama kutaka kudhuru viongozi.

Sheria haiangalii kiongozi wa chama, ni vema mahakama iachiwe uhuru wa kutoa maamuzi yake. Kwa nini hofu ijengwe. Ni watu wangapi Tanzania hii wameshitakiwa, hadi Mawaziri Mramba na Yona wakati huo wa Kikwete walishitakiwa na kupata adhabu. Alie kuwa mkuu wa Wilaya Hai ameshitakiwa na kufungwa miaka 30 na bado ana kesi. Mtu akitenda kosa ana haki ya kushitakiwa bila kuangalia wadhifa wake. Isipokuwa wale walio na kinga tu kwa mujibu wa sheria. Tena hata wao baadae inabidi washitakiwe, hii sheria iondolewe.

Tuache ushabiki, maslahi ya nchi lazima yalindwe. Si kila jambo tulichukulie kisiasa. Umetenda kosa utashitakiwa bila kujali wadhifa wako. Hakuna mtu mwenye uhalali wa kuvunja sheria nchi hii. Sweka ndani wote! Awe wa CCM, awe wa Chadema, Awe CUF hata ACT-Wazalendo na wengineo.
 
Hadi hapa Mbowe Sio Gaidi Ila Ni Visa Tuuu, sio Kila Mtu atakuheshimu, Jiulizeni hadi mbowe hajawaheshimu kwanini? Mngesema kuwa Mbowe amehukumiwa kwa kutokuwa na Heshima na Sio kumwambia Mtu Gaidi.

Wazungu waliona mbali ndio maana wakaacha kwenda kwenye Kesi. Ila AFRIKA kuja Kuendelea Ni Lazima Tutawaliwe Tena. Mtu anang’ang’ania Heshima.
 
Siku Mbowe akitoka kabla hajaongea chochote waandae kongamano la katiba na siku ya kwanza aongee akiwa kwenye kongamano
Hii italeta atention kwa wananchi na dunia
Na pia watakuwa hawana la kumfanya kwa wakati huo
Kama suala lilikuwa ugaidi na si katiba itafahamika
 
Maneno aliyosema mh rais si sawa, ingekuwa Mbowe kesha hukumiwa angekuwa sahihi. Rais kesha mhukumu Mbowe, na hii si mara ya kwanza, hata alipo hojiwa na BBC alionesha shauku hiyo. Ashukuru tuna mahakama zinazoongozwa na dola, angeaibika.
 
Thubutu yako. Never underestimate a woman in power. Kwanza amemuonyesha kuwa she can na ndiyo maana mnalia lia kila mahali aachiwe. Kama Mbowe ni mwamba akae kimya asbiri Mahakama. Na hizi Mahakama zilizomhukumu Sabaya na zikaonekana huru, msianze kusema ooh haziko huru sababu ya huyo DJ wenu. And alitoka I swear ataufyata, wacha michezo na Serikali
 
Rais akizungumz kama Mkuu wa Executive sio state anawez kumtambua mtu yeyote alifikishwa Mahakamani kwa kosa la Jinai kama Mhalifu kwa kuwa upande wake (Serikali) ndio unatuhumu na kupeleka kesi mahakaman kama ambavyo upande unaotuhumiwa unaweza kutambua Mashtaka kama mashtaka ya kubambikiza


Kama una haki ya kutambua kesi ya Mbowe kuwa ya kubambikiwa basi na mwingine ana haki ya kutambua mashtaka hayo hayo kama mashtaka ya kweli

Kuna watu wanaamini wao wana haki ya kumkosoa Rais ila Rais hana haki ya kuwakosoa
 
Mbona umerejea kwa sabaya,au alikuvamia ukaona raha?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
mtihani huu, ccm wamejisahau wanajifananisha na yesu eti nchi hii ni mali yao pumbafu sana
 
Mama aliona Mbowe kama anataka kumpanda kichwani kwa kampeni yake ya katiba mpya.

Hapa inadhihirisha tuhuma za Mbowe ni za kubumba.... Na pia kumwonyesha tu kuwa huwezi kushindana na serikali
HUKO WAPI Stuxnet the witch? Njoo usome hii comment wewe mchawi NAKUCHUKIAGA SANA.
 
Kuzitii mamlaka na kuziheshimu..

Mamlaka au Dola ndio inacontrol kila jambo katika Taifa kupitia vyombo vyake, Dola kupitia vyombo vyake ina taarifa ya kila jambo linaloendelea hapa Tanzania kuliko mtu yeyote..
Kupitia taarifa hizo Dola ndio pia inapata nguvu ya kulinda mipaka na kutulinda humu ndani..

Dola kupitia vyombo vyake inaposema hili kwasasa lisifanyike na twende na uelekeo huu halafu ikatokea tofauti HAPO UTAKUWA UMESHINDWA KUIHESHIMU DOLA, kujaribu kuipa dola mashinikizo ya kisiasa wakati yenyewe kupitia vyombo vyake inajua position ya nchi kwa sasa iko hapa na kuliachia hili tutafika pale, UKAJARIBU KULAZIMISHA KWA NGUVU HOJA ZA KISIASA ni kutokuiheshimu dola na kukosa usikivu..m
 
Tuhuma za Mbowe na mashtaka dhidi ya Mbowe ikiwemo watuhumiwa wenzie mchakato huo umeanza tangu Samia akiwa Makamu wa Rais
Mama aliona Mbowe kama anataka kumpanda kichwani kwa kampeni yake ya katiba mpya.

Hapa inadhihirisha tuhuma za Mbowe ni za kubumba.... Na pia kumwonyesha tu kuwa huwezi kushindana na serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…