Yaani univunjie hotel niliyokuwa napata riski yangu
Yaani unifyekee bustani yangu ya mbogamboga iliyokuwa inanipa riski yangu
Yaani unifungie account zangu za benki zote ambazo nilikuwa naweka akiba zangu kwa miaka.
Yaani uniweke ndani miezi minne kwa kosa la kuandamana na kusababisha kifo cha akwilina..
Yaani watu naowaongoza uwaumize, uwape kesi za kubambika kukomoana
Yaani ukanivunja mguu wangu, nikajitibia nikapona..sikukata tamaa
Yaani wagombea wetu 60% uwateke, uwanyike sifa za kugombea bila sababu za msingi..
Yaani mawakala wetu uwazuie nje na wakitaka kuingia unawafungulia kesi ya vurugu kituo cha uchaguzi
Yaani viongozi wenzangu wapotee, waumizwe wengine wabakie vilema huku naona...
Kwa yote haya nikapiga kifua changu nikamwambia MUNGU wangu ayasamehe- nikasamehe.... Baada tu ya Urais wako nikaja kwako kwa unyenyekevu mkubwa nikakuomba tukutane tuyajadili kwa kina ili tufikie muafaka ama maridhiano ya kitaifa - ukawa kimya kwa maana nyingine hukutaka.
Leo umenipa kesi ya UGAIDI, nasota gelezani ni sawa , ila kweli leo unaniambia nini sina HESHIMA, kweli ndugu ?? Hapana, kwa hili hapana Hapana umenikosema sana.