Rais Samia: Don't rock the boat. Biashara na uchumi vitayumba

Wewe unataka CDM wafanye vurugu na kuleta taharuki waachiwe tu na sheria isifuate mkondo wake? Huo ni ujinga, unataka serikali ianze kuogopa watu kisa wawekezaji? Mwisho wa siku unataka tuwe na serikali kama za Haiti, Jamaica na sehemu hizo za hovyo ambazo serikali inaogopa watu na taasisi zake?? Hilo haliwezekani, hao wawekezaji waondoke tu.

SSH muongo.elewa ivo
 
Mkuu nakushukuru kwa kunielewa.
Mfanyabiashara ni mtu anayejenga capital yake kwa jasho.
Hana muda wa kazi
Hana wa kumlalamikia biashara ikifa
Hana overtime za kudai
Hana pensheni ya kuidai serikali
Hana wa kumlalamikia uchumi ukianguka na biashara ikadoda

Lakini,
Anawajibu wa kulipa kodi zote za TRA(zinafikia 56)
Anawajibu wa kulipa wafanyakazi
Anawajibu wa kuilipa serikali kwa kuajiri wafanyakazi utafikiri serikali inahodhi watu (NSSF,WCF,SDL n.k.)
Anawajibu wa kumlipa mfanya kazi hata akiongeza dakika moja ya kazi
Ana wajibu wa kulipa tozo za LATRA,BIMA, n.k.(na tozo-kodi nyingine nyingi kulingana na aina ya biashara)

Sasa mkuu Kalamu1 kwa nini nisiwe na ubinafsi wa kulinda mtaji wangu?
Wewe unaanza kazi saa mbili, kwa unakula chai saa nne kwa saa nzima.
Chakula mchana lisaa lizima.
Mchana unaendanda nje ya ofisi" kusimaia mambo yako muhimu" yasiyo ya kiofisi kwa masaa mawili.
Hiyo ni ratiba yako ya kila siku!
Halafu mshahara wako uko palepale !
Ukichelewa mshahara kwa kazi ambayo hukuifanya inakuwa valangati, hadi vyombo vya habari vitaitwa
Huyo ndo mtu wa mshahara-anapo pa kuegemea !

Sasa hapo wewe na mimi tutafananaje?

Silver chance ya kupata mbia ikiponyoka kwa sababu uncertainities zinazotokana na political adventures kwa nini tusilalamike?

Wewe mshahara wako uko pale pale!!!
EeeenHeeee, mkuu wangu 'masopakyindi', umenipa za uso ambazo kwa hakika sizistahili kabisa!

Ngoja nikueleze kwa nini unakosea.

Mimi, sio "mfanya kazi anayepokea mshahara" kama unavyodai hapo juu. Sijui ni wapi ulipopata habari ya mimi kuwa mwajiriwa serikalini.

Kwa hiyo, hayo yote ya kufaidi kama mfanyakazi uliyoandika hapo juu, mimi sifaidiki nayo kabisa, pamoja na kwamba, hata kama ningekuwa ni mmoja wa wanaotegemea mshahara, pia ningeweza kukujibu kukuonyesha kwamba madai yako ya hao wafanyakazi kufaidi siyo ya kweli.

Mimi ni mmoja kati ya kundi kubwa zaidi hapa nchini, ambalo manufaa tunayoyapata toka serikalini ni madogo zaidi kuliko kundi lingine lolote, pamoja na wingi wetu, takribani zaidi ya asili mia 65, kama siyo zaidi, kwa wingi wetu; na mchango wetu katika uchumi wa taifa ni mkubwa kuliko yanavyoingiza makundi mengine yoyote.

Mimi ni mmoja wa wakulima wadogo wadogo, na kidogo nina mifugo kadhaa, si zaidi ya ng'ombe kumi (ng'ombe wa asili). Kilimo changu ni cha ekari tano, sina uwezo wa zaidi ya hapo.

Wewe unajivunia sana kulipa hizo kodi serikalini, ukidhani unatunufaisha hata sisi wakulima wadogo, dhana ambayo ni potofu kabisa.
Matatizo yetu ya miaka yote nchini mwetu yanafahamika. Miaka sitini sasa tokea uhuru, nchi yetu hata mbegu tu zilizobora kutusaidia kwenye kilimo chetu ni jambo lisilowezekana. Nyinyi wafanya biashara mnapopewa upendeleo muagize mbegu bora toka nje, bei zenu hatuziwezi, mbolea hivyo hivyo, wataalamu wa kutusaidia kwenye kilimo, ni matatizo tupu.

Sasa wewe, leo hii na biashara zako, unajiona wewe kwamba unastahili zaidi, kwa vile tu unapata upendeleo kwa hao wakubwa walioko serikalini, na chama chako, CCM, ambacho bila shaka sababu yako ya kuendelea kuwa huko ni kutokana na mafao mnayoyapata kwenye biashara zenu, leo hii unapata ujasiri wa kuja hapa na kujionyesha kwamba nyinyi wafanya biashara ndio mnaostahiri keki kubwa zaidi ya taifa hili?
Kwa nini, vijisenti mnavyowapa huko CCM, na wao wanapo kula na kusaza, na kututupia sisi magwanda ya kijani ya CCM ndio mnayoichukulia kuwa ndiyo bei sahihi ya utu wetu?

Mkuu 'Masopa', nimesoma mengine uliyoandika humu na kujibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwa hayo uliyoandika kwenye mada hii. Hakika umejifunua zaidi kuliko nilivyowahi kukusoma tangia nikufahamu kwa humu JF. Huu ubinafsi umekuelemea kiasi kwamba uko radhi kumtumikia shetani mradi tu anakunufaisha wewe, hata kama atakuwa anawaumiza ndugu zako.

Sote tunataka manufaa binafsi tuyapate, lakini haya hayawezi kuwa manufaa ya kweli kama taifa letu kwa ujumla linaumizwa.

CCM unayodai wewe ni mwanachama wake imegeuka kuwa adui mkubwa wa nchi yetu kwa mienendo inayoifanya sasa hivi. Kujitangaza wewe ni mwanachama wakati huu, sijui kunakupa sifa gani, na hasa unapoonekana kuunga juhudi za viongozi wanaolikandamiza taifa letu.
 
Kwanza nina declare position,
Mimi ni mwana CCM.
Tena ni mfanya biashara.
Zaidi ya hapo nina muunga mkono Mama Samia.

Haya matukio ya kisiasa hivi karibuni kibiashara na hatimaye kiuchumi yameleta ukakasi kidogo.

Nasema hivi kwa experience ya yaliyonikuta hivi karibuni.

Nilipata ahueni sana kibiashara baada ya Mama Samia kutamka wazi kuwa yuko pro-business.
Nilimpata partner toka nje aliyekubali kuwekeza pamoja na mimi, mtaji wangu ukiwa industrial plot na vibali vyote vya uwekezaji.

Na hao jamaa walishakuja, sitataja uraia wao.

Mara tukaanza kusikia maneno ya ugaidi na watu kuswekwa ndani.

Ieleweke, sitetei uhalifu wa aina yoyote, lakini ijulikane kuwa ukijitangaza ugaidi watu hasa wawekezaji wanasita.

To make my story short, muwekezaji wangu kasitisha uwekezaji kwa muda, anasema anaangalia na ku assess situation.
Kwangu mimi ni big set back, maana time is money and a missed oppurtunity is a loss.

Mama Samia charanga karata vizuri, tunahitaji mtaji wa tranquility.
Kiukweli kujitangaza kuwa Tanzania Kuna ugaidi Ni upuuzi wa Hali ya juu kabisa, inaitia Nchi Doa kabisakabisa, sijui mama Nani kamshauri hii kitu kwa kujitangaza tuna ugaidi na magaidi wamekamatwa
 
Kwanza nina declare position,
Mimi ni mwana CCM.
Tena ni mfanya biashara.
Zaidi ya hapo nina muunga mkono Mama Samia.

Haya matukio ya kisiasa hivi karibuni kibiashara na hatimaye kiuchumi yameleta ukakasi kidogo.

Nasema hivi kwa experience ya yaliyonikuta hivi karibuni.

Nilipata ahueni sana kibiashara baada ya Mama Samia kutamka wazi kuwa yuko pro-business.
Nilimpata partner toka nje aliyekubali kuwekeza pamoja na mimi, mtaji wangu ukiwa industrial plot na vibali vyote vya uwekezaji.

Na hao jamaa walishakuja, sitataja uraia wao.

Mara tukaanza kusikia maneno ya ugaidi na watu kuswekwa ndani.

Ieleweke, sitetei uhalifu wa aina yoyote, lakini ijulikane kuwa ukijitangaza ugaidi watu hasa wawekezaji wanasita.

To make my story short, muwekezaji wangu kasitisha uwekezaji kwa muda, anasema anaangalia na ku assess situation.
Kwangu mimi ni big set back, maana time is money and a missed oppurtunity is a loss.

Mama Samia charanga karata vizuri, tunahitaji mtaji wa tranquility.
Tatizo ni definition yako ya tranquility ni tofauti na ya Sa100.
 
Mama amehamua afanye yale ambayo SUKUMA GANG walikuwa wanayataka afanye, kwa kifupi mama muoga
 
EeeenHeeee, mkuu wangu 'masopakyindi', umenipa za uso ambazo kwa hakika sizistahili kabisa!

Ngoja nikueleze kwa nini unakosea.

Mimi, sio "mfanya kazi anayepokea mshahara" kama unavyodai hapo juu. Sijui ni wapi ulipopata habari ya mimi kuwa mwajiriwa serikalini.

Kwa hiyo, hayo yote ya kufaidi kama mfanyakazi uliyoandika hapo juu, mimi sifaidiki nayo kabisa, pamoja na kwamba, hata kama ningekuwa ni mmoja wa wanaotegemea mshahara, pia ningeweza kukujibu kukuonyesha kwamba madai yako ya hao wafanyakazi kufaidi siyo ya kweli.

Mimi ni mmoja kati ya kundi kubwa zaidi hapa nchini, ambalo manufaa tunayoyapata toka serikalini ni madogo zaidi kuliko kundi lingine lolote, pamoja na wingi wetu, takribani zaidi ya asili mia 65, kama siyo zaidi, kwa wingi wetu; na mchango wetu katika uchumi wa taifa ni mkubwa kuliko yanavyoingiza makundi mengine yoyote.

Mimi ni mmoja wa wakulima wadogo wadogo, na kidogo nina mifugo kadhaa, si zaidi ya ng'ombe kumi (ng'ombe wa asili). Kilimo changu ni cha ekari tano, sina uwezo wa zaidi ya hapo.

Wewe unajivunia sana kulipa hizo kodi serikalini, ukidhani unatunufaisha hata sisi wakulima wadogo, dhana ambayo ni potofu kabisa.
Matatizo yetu ya miaka yote nchini mwetu yanafahamika. Miaka sitini sasa tokea uhuru, nchi yetu hata mbegu tu zilizobora kutusaidia kwenye kilimo chetu ni jambo lisilowezekana. Nyinyi wafanya biashara mnapopewa upendeleo muagize mbegu bora toka nje, bei zenu hatuziwezi, mbolea hivyo hivyo, wataalamu wa kutusaidia kwenye kilimo, ni matatizo tupu.

Sasa wewe, leo hii na biashara zako, unajiona wewe kwamba unastahili zaidi, kwa vile tu unapata upendeleo kwa hao wakubwa walioko serikalini, na chama chako, CCM, ambacho bila shaka sababu yako ya kuendelea kuwa huko ni kutokana na mafao mnayoyapata kwenye biashara zenu, leo hii unapata ujasiri wa kuja hapa na kujionyesha kwamba nyinyi wafanya biashara ndio mnaostahiri keki kubwa zaidi ya taifa hili?
Kwa nini, vijisenti mnavyowapa huko CCM, na wao wanapo kula na kusaza, na kututupia sisi magwanda ya kijani ya CCM ndio mnayoichukulia kuwa ndiyo bei sahihi ya utu wetu?

Mkuu 'Masopa', nimesoma mengine uliyoandika humu na kujibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwa hayo uliyoandika kwenye mada hii. Hakika umejifunua zaidi kuliko nilivyowahi kukusoma tangia nikufahamu kwa humu JF. Huu ubinafsi umekuelemea kiasi kwamba uko radhi kumtumikia shetani mradi tu anakunufaisha wewe, hata kama atakuwa anawaumiza ndugu zako.

Sote tunataka manufaa binafsi tuyapate, lakini haya hayawezi kuwa manufaa ya kweli kama taifa letu kwa ujumla linaumizwa.

CCM unayodai wewe ni mwanachama wake imegeuka kuwa adui mkubwa wa nchi yetu kwa mienendo inayoifanya sasa hivi. Kujitangaza wewe ni mwanachama wakati huu, sijui kunakupa sifa gani, na hasa unapoonekana kuunga juhudi za viongozi wanaolikandamiza taifa letu.
Ninachoweza kukushauri tu ni kwamba dunia ni struggle.
Soma zaidi juu ya filosofia ya biashara, na uta gundua kuwa kivutio chake kikubwa ni profit.

Sasa wewe ukiita hilo kuwa ni ubinafsi, basi nawe ukilima gawa mazao yako yote kila mwaka uanze upya kila msimu, na ujipime utafikia wapi.
In short, effort must be beneficial katika mazingira yoyote.
Nchi hii ni biashara zina misingi ya kibepari, tofauti na ujamaa uliofilisi nchi miaka ya Mwalimu.
 
Naona hatuelewani, au hutaki tu kuelewa.

Mimi mazao yangu kila mwaka ni kama nagawa tu, na hasara kubwa inatokana na ukandamizaji mnaonifanyia nyinyi wafanyabiashara. Hivi hata hili unataka nikasome 'filosofia' juu yake?

Kila mwaka mimi mkulima "ninaanza upya", siyo "kama ninaanza upya"; ndiyo maana maisha yangu na wengi wenzetu hali zetu hazibadiliki tokea uhuru 12961!
Of course, "effort must be beneficial' katika mazingira yoyote'", sasa kama unatambua hivyo, kwa nini wewe mfanya biashara ndiye ujione kuwa ndiye mwenye haki zaidi ya sisi wakulima, na hata hao wafanyakazi unaowabeza hapa!

Ni mawazo potofu kudhani kwamba ni "ujamaa" ndio sababu Tanzania ni maskini kama ilivyo sasa hivi. In fact siyo upotofu tu peke yake, bali ni kasumba inayotumika na watu wavivu wa kutumia akili.
 
Sasa kama zoezi unalifahamu, unajua unaibiwa, na bado hubadiliki, nani alaumiwe?
Sisi tunatumia formula ya MONEY BEGETS MONEY!

M+Mv=M'

M= Money starting capital
Mv= Add value to the Money
M'=Money at greater value including profit.

Sasa mkuu hii formula usipo iheshimu lwako.
Sisi tumefundishwa hii 2nd Year miaka mingi iliyopita.
Tumeitumia hii kanuni na kuiheshimu,na imetuheshimu.
 
Anayestahili lawama ni watu kama wewe, ambao kazi kubwa mnayofanya ni kuwarubuni hao CCM, huku mkiwasifu kwa maovu yao ili wazidi kutukandamiza.

In short, nyinyi mmekuwa ni sehemu muhimu sana ya ukandamizaji wa haki zetu, na ndiyo maana mnarundikana huko CCM na kutetea yasiyostahiri kutetewa kwa sababu tu ya shibe zenu.

Maisha ya waTanzania hayawezi kuishia kwenye vi'formula' kama hivyo unavyoviweka hapa. Hawa watu utu wao unayo thamani zaidi ya hayo unayoyalilia kuwa ndiyo thamani ya uhai wako.
 
Dua la kuku hio brother!
Fanya kazi kwa akili upate maendeleo yako na acha kutafuta scape goats au unyasi wa kukusaidia.
 
Dua lipi tena!

Kazi ninayofanya ingeniwezesha kupata maendeleo makubwa pasingekuwepo na watu wa aina yenu mnaokwamisha juhudi zetu. Lakini najuwa tutafika tu kwa sababu hamuwezi kuzuia kujikomboa kwetu hata mhangaike vipi.
 
Kwanza nina declare position,
Mimi ni mwana CCM.
Tena ni mfanya biashara.
Zaidi ya hapo nina muunga mkono Mama Samia.

Haya matukio ya kisiasa hivi karibuni kibiashara na hatimaye kiuchumi yameleta ukakasi kidogo.

Nasema hivi kwa experience ya yaliyonikuta hivi karibuni.

Nilipata ahueni sana kibiashara baada ya Mama Samia kutamka wazi kuwa yuko pro-business.
Nilimpata partner toka nje aliyekubali kuwekeza pamoja na mimi, mtaji wangu ukiwa industrial plot na vibali vyote vya uwekezaji.

Na hao jamaa walishakuja, sitataja uraia wao.

Mara tukaanza kusikia maneno ya ugaidi na watu kuswekwa ndani.

Ieleweke, sitetei uhalifu wa aina yoyote, lakini ijulikane kuwa ukijitangaza ugaidi watu hasa wawekezaji wanasita.

To make my story short, muwekezaji wangu kasitisha uwekezaji kwa muda, anasema anaangalia na ku assess situation.
Kwangu mimi ni big set back, maana time is money and a missed oppurtunity is a loss.

Mama Samia charanga karata vizuri, tunahitaji mtaji wa tranquility.
Huwezi kuchukua kesi yako moja (kama ni kweli napo) kujaribu kujenga hoja juu ya mazingira ya kisiasa yaliyopo nchini na mustakabali wa uwekezaji.

Usifikiri wawekezaji serious ni watu wa mchezo mchezo kwamba wakiwa na maslahi na kitu fulani watatishwa na michezo ya kuigiza ya wanasiasa.

Huyo partner wako ni mwekezaji kanjanja au kuna jambo jingine nyuma ya pazia ambalo hajakwambia. Wenzako wanawekeza hadi Afghanistan seuze nchi bora kabisa kiuwekezaji kama Tanzania?
 
Back
Top Bottom