Scapegoating kama kawa. Wakati ule mkasema maduka yanafunga kisa Magufuli. Leo mnasema maduka yanafunga kisa Samia. Kuna jirani yangu hapa kafunga duka lake. Asingekuwa jirani nnayemfahamu kindakindaki na kufahamu pia kisa cha kufunga pengine nami ningeamini sababu ni Magufuli au Samia.
Tukirudi kwenye mada. Hakuna mazingira yoyote hapa Tanzania yatakayomfanya mwekezaji origino aliyejipanga na anayejua nini anataka kufanya atashindwa kuwekeza. Au kwa nini unadhani wachina wameweza kupenya hadi sehemu za ndani ndani humu Tanzania na kufungua tuviwanda vyao na wanapeta tu? Ni kwa sababu hawana tyme na power plays za wanasiasa. Wana skills, wana capital, wana business plan, wamecalculate risk-to-benefit ratio na wana vibali vyote vya kiserikali vya kufanya biashara. And they are winning!
Ukiona mtu anatanguliza issues zingine tofauti na issue kuu iliyo mezani ujue ana lake jambo. Usipoteze muda na watu wa aina hiyo.