BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Amezungumia utekelezaji wa report ya CAG? vipi vijana walio jazana mtaani bila ajira kasemaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
anaongea vitu vyepesi tupu, huwezi msikia anaongea mambo magumu,huwezi sikia swala la ufisadi wala ajira wala, gharama za maisha, hivyo hutakaa uvisikie kutoka kinywani mwake. Sukari kwa sasa ni Tsh 4000/ kilo 1 huwezi msikia anazungumzia hayo.Tumepigwa aise
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa salaam za mwaka mpya leo tarehe 31 Desemba, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema changamoto ya upungufu wa umeme unaosababisha mgawo nchini utaisha baada ya mradi wa bwawa la Julius Nyerere utakapoanza kufanya kazi.
Aidha Rais Samia amesema, Februari mwaka 2024 watawasha mtambo wa kwanza kisha Machi kuongeza mtambo wa pili, mitambo hiyo itatoa umeme Megawati 470 hivyo utafidia upungufu wa Megawati 300 uliopo sasa.
“Habari njema ni kwamba, panapo majaliwa, mwezi Februari 2024 tutawasha rasmi mtambo wa kwanza na mwezi Machi tutawasha mtambo wa pili. Mitambo hii miwili itatupatia jumla ya Megawati 470 na hivyo kufidia upungufu wa sasa ambao ni Megawati 300 tu. Hatua hii itakwenda sambamba na kuwasha mtambo wa Rusumo utakaoongeza Megawati 27.”
“Ni imani yangu na Serikali kwa ujumla kuwa, hatua hizi zitaleta ufumbuzi wa kudumu kwa suala la mgao wa umeme nchini. Aidha, Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vyanzo vingine vya umeme kama vile gesi, jua, na upepo, ili kuongeza uhakika wa umeme,”amesema na kuongeza Rais Samia.
RELI YA SGRRais Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa wanaohusika na mradi wa reli ya kisasa (SGR) kuhakikisha inapofika Julai 2024 safari za kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma zinaanza.
“Nimekuwa nikisikia mabadiliko ya tarehe za kuanza kwa safari za treni, na kwa kweli, wananchi wamechoshwa na vijisababu, wanataka kuona reli ikifanya kazi. Sasa, naelekeza, ifikapo mwisho wa Julai 2024, safari kati ya Dar es Salaam hadi Dodoma zianze,”amesema Rais Samia.
AMANI, ULINZI NA USALAMAMipaka yote ya nchi yetu iko salama, na Muungano wetu unazidi kuimarika. Aidha, vikosi vyetu vya ulinzi na usalama vipo imara. Sote tulishuhudia namna vikosi vyetu vilivyojitoa katika uokoaji na kurejesha hali ya kawaida pale tulipopatwa na maafa. Nitumie fursa hii kuvipongeza kwa ujasiri na uzalendo wao.
MAPITIO YA KIUCHUMIKatika kuuhami uchumi wetu, tulitekeleza sera madhubuti za fedha ili kuhakikisha utulivu wa bei, kuchochea ukuaji na kudumisha uthabiti wa sekta ya fedha.
Aidha, ukuaji wa Uchumi na Pato la Taifa kwa mwaka 2023 ulikadiriwa kuongezeka kwa 5.2% ikilinganishwa na 4.7% mwaka 2022.
Tumeendelea kudhibiti mfumuko wa bei, ambao katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2023 ulipungua hadi wastani wa 3.9%, ikilinganishwa na wastani wa 4.3% kipindi kama hicho mwaka jana, 2022.
SEKTA YA KILIMOTumeongeza bajeti ya kilimo kutoka Shilingi Bilioni 751 mwaka jana hadi Shilingi Bilioni 970 mwaka huu, sawa na ongezeko la 29%. Shabaha yetu ni kuchochea kiwango cha ukuaji wa sekta ya kilimo kufikia 10% kwa mwaka, ifikapo mwaka 2030.
Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 17,148,290 msimu wa 2021/2022 hadi tani 20,402,014 msimu wa mwaka 2022/2023, hivyo kufikisha 124% ya kiwango cha utoshelevu chakula nchini.
Serikali imetoa shilingi bilioni 116 kwa NFRA na CPB ili kuchochea soko, ambapo katika awamu ya kwanza NFRA imenunua jumla ya tani 200,293 za mazao. Vilevile, tumeanzisha mnada mpya wa zao la chai.
Hadi Novemba, 2023 tani 204,818.16 za mbolea zilikuwa zimesambazwa kwa wakulima katika mikoa yote ya Tanzania Bara, ikiwemo ruzuku ya serikali yenye thamani ya shilingi Bilioni 67.82.
Serikali imeendelea na jitihada za kuwaingiza vijana na wanawake kwenye uzalishaji, ikiwemo kwa kutenga jumla ya ekari 201,241.6. Aidha, imeanzisha programu ya kilimo cha kisasa iitwayo Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ili kuongeza uzalishaji, kuchochea viwanda vya usindikaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
Yaani wewe umeishiwa point mpk unasubiri mtu mwingine akutolee hizo point!Tumepigwa aise
Ni wazo zuri mkuu ngoja tuupokee mwaka kwanzaKwanini usiagize Konyagi ujipongeze kwa Mwaka mpya kuliko kisikiliza Mwanasiasa na hadaa zao?
Nenda Chattle kaburini........hotuba haina mashiko.....kabisaa
$1 lazima ifike 5000 tshNi kosa kubwa sana Rais anapokiri kuwa dollar hakuna…ni juzi tuu BOT walisema dollar zipo! Maana yake tujiandae dolla kupanda mara dufu maana Rais amehalalisha hata waliozificha wanapata uhalali kabisa!
Kaongelea achievement tu ambazo zimejaa siasa tupu ukimsikiliza utadhani Tanzania ni nchi ya asali na maziwa kumbe wananchi wanatabika kwa gharama ya maisha kuwa juuanaongea vitu vyepesi tupu, huwezi msikia anaongea mambo magumu,huwezi sikia swala la ufisadi wala ajira wala, gharama za maisha, hivyo hutakaa uvisikie kutoka kinywani mwake. Sukari kwa sasa ni Tsh 4000/ kilo 1 huwezi msikia anazungumzia hayo.
Sijawahi msikia akizungumzia mambo serious ya nchi hii.Kaongelea achievement tu ambazo zimejaa siasa tupu ukimsikiliza utadhani Tanzania ni nchi ya asali na maziwa kumbe wananchi wanatabika kwa gharama ya maisha kuwa juu
Inahuzunisha na kusikitisha sana