Asome vile vile na namba 15 inayo husu masuala ya Mafuta na mali asili - mwishoni mwa mwaka jana si nilimsikia Dk.Shein kama sikosei akisema utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi Baharini karibu na Zanzibar ni suala la Serikali ya mapinduzi Zanzibar na si la muhungano - alitoa impression as if Serikali mbili zimefikia makubaliano kwamba mafuta/gesi itakayo patikana/chimbwa Zanzibar ni mali ya Wazanzibari Serikali ya Muhungano haiwahusu!!
Hili waliliondoa mapema baada ya kusikia kuna mafuta na gesi. Walichotaka ni kuwa rasilimali zao zisitumike katika muungano. Hapa chini umeeleza vizuri sana
Lakini umeme utakao zalishwa Bwawa la Rufiji ni mali ya muungano, Revenue zinakazo kuwa generated na mradi wa ufasirishaji wa crude oil kutoka Uganda kuja Bandari ya Tanga - hizo ni revenue za muungano lazima zigawiwe nusu kwa nusu, nisijue fedha za gesi ya Songo songo zinagawanywaje, dhahabu ya Geita, Almas ya Mwadui,Karafuu ya Zanzibar, Mwani nk.
Binafsi uwa napata wakati mgumu kuelewa kinacho endelea nyuma ya pazia, mengi yaliyo andikwa kwenye makaratasi/kanuni za makubaliano ya muungano wala hayawekewi maanani - miaka 50+ bado tunazungumzia kero za muungano, sio matatizo bali "KERO" hii wapi na wapi??
Kwakweli inasikitisha sana. Si hayo tu kuna mengi sana
1. Wametaka 21% ajira za muungano. Katika hiyo 21% ajira wanazopata Wazanzibar hazihusu mambo ya muungano. Kwa mfano, Mzanzibar anaajiriwa TAMISEMI, Wizara ya maji, Mawasiliano, Mifugo n.k. kwa sababu zipi
Lakini pia wanataka waajiriwe katika taasisi zisizo za muungano kama TBS wakati kuna ZBS
Kwa Zanzibar 21% ya ajira za muungano ni nyingi kuliko ajira za SMZ.
Licha ya fadhila hizo za ajira bado wanalipwa na JMT ambayo pesa zake zinatoka hazina Dar.
Hakuna ushahidi wowote wa Zanzibar kuchangia muungano kwa miaka takribani 40 sasa.
Kuna masuala ya gharama za muungano. Hapa hutawasikia Wazanzibar wakieleza nini mchango wao
Mathalani, wanachangia nini katika kuendesha wizara ya mambo ya nje! Lakini utawasiki wanataka nafasi sawa za uteuzi katika ubalozi.
Kuna suala la Wabunge! Ikiwa tunasema asilimia 4% ya mapato ya BoT ambayo ni mapato ya rasilimali na kodi za Watanganyika iende Zanzibar, ni vipi basi SMZ haihudumii wawakilishi wanaokuja Dodoma Bungeni?
Wale Wazanzibar wapo Bungeni kwa ajili ya Zanzibar katika mambo yasiyozidi 7. Kwanini Hazina Tanganyika ibebe mzigo wa kuwahudumia ?
Elimu ya Juu: Hili si suala la muungano. Kuna HESLB na ZHESLB . Kwanini basi HSELB ya bara iwape 'msaada; na si mkopo wanafunzi wa Zanzibar kwa wingi zaidi kuliko mkopo unaotolewa na ZHESLB?
Kuna suala la Akaunti ya pamoja ya fedha. Ukiuliza ni ya nini , Wazanzibar watakwambia ni ya kugawana misaada na fedha. Hakuna Mzanzibar atakayekuambia akaunti hiyo ni ya kuchangia na kutoa! hapana! wao ni kutoa tu
Zanzibar ina watu milioni 1.2 na nusu yao wanaishi Tanganyika. Kwa maana kwamba at anytime Zanzibar inakuwa na approx. watu laki 600. Kwa mwendo huu wa kuchota , sidhani kam wanasababu ya kufanya kazi.
Hawana sababu ya kufanya kazi kwasababu kadri mnavyolipa kodi bara, mnavyotumia rasilimali zenu wao wana mtego wa 4% . Sasa piga hesabu ya 4% ya pato la watu milioni 50 wa Tanganyika!
Suluhu hapa ni moja turejee katika rasimu ya Warioba, mambo 7 tu! mengine kila nchi ijishughulishe
Tanganyika inatoa resources nyingi sana kwenda kuhudumia eneo ambalo kwa Tanganyika ni jimbo moja la uchaguzi, huku tukiacha maeneo yanayochangia sana katika Pato la Taifa bila resources. Ni kwa dividend or return gani? Nani wa kumsemea ''Tanganyika'?
Tunabeba lawama za bure kwa fadhila tunazotoa. Je, haitoshi?
Kwasasa ''Changu ni Chetu, chako ni chako'' na hii ifike mwisho.
JokaKuu Pascal Mayalla Ngongo