S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,689
- 7,145
Rais Samia: Fikiria Hatua Sahihi kwa Maslahi ya Taifa na Familia Yako Pia.
Katika siku za hivi karibuni, inavyoonekana katika jicho la pembeni kwamba kumekuwa na mjadala mkali kuhusu mustakabali wa uongozi ndani ya Chama chako cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, hasa kutokana na mienendo ya baadhi ya viongozi waliobaki kama urithi kutoka awamu ya tano ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Hoja zifuatazo hapa chini zinaashiria umuhimu wako kama wewe Raisi wetu- Samia Suluhu Hassan kufanya maamuzi magumu lakini ya busara kwa wakati huu.
kwanini ni busara kama wewe Rais Samia kuangalia uwezekano wa kuachia ngazi kwa amani, ili kulinda heshima yako, ustawi wa familia yako na mustakabali wa taifa kwa ujumla wako:
1. Viongozi wengi wa awamu ya Magufuli wana ajenda zao hata kama wako kimya – wanapima upepo:
Rais Samia bado una nafasi kubwa ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu. Uamue kwa busara, kwa ajili ya amani yako binafsi, familia yako na taifa kwa ujumla, hutakuwa wa kwanza wala wa mwisho kufanya hivyo.
Sio kuchelewa na waka hauta chelewa. Ukiamua sasa, Utaacha urithi wa kipekee wa kiongozi wa kwanza mwanamke aliyesimamia mpito wa kisiasa kwa utulivu na hekima.
Povu ruksa. Mjumbe hauwawi- message sent and delivered

- Wengi wa viongozi waliolelewa na kupewa nafasi kubwa wakati wa awamu ya Magufuli wanaonekana bado kushikilia misimamo na mikakati yao ya zamani.
- Kuna ishara kwamba wanajaribu kurejesha baadhi ya sera na mitazamo iliyotamalaki wakati huo, jambo ambalo linaweza kuleta msuguano na dira mpya unayoijenga Rais Samia.
- Mwisho wa siku, Rais Samia unaweza kuishia kupambana na kundi lako mwenyewe ndani ya chama, hali itakayochochea migawanyiko mikubwa.
- Kama hali hii haitadhibitiwa mapema, kuna uwezekano mkubwa wa machafuko ya ndani ya chama kuibuka hadharani.
- Kelele za kisiasa zitakua kubwa, zitaathiri utulivu wako wa akili na kufanya kuongoza taifa kuwa jambo gumu mno.
- Badala ya kutumia muda wako katika kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia, Rais Samia utaishia kuzima moto wa migawanyiko isiyoisha.
- Hii itakuwa njia ya kuonesha ukomavu wa kidemokrasia ndani ya chama na pia kutoa nafasi kwa damu mpya yenye kukubalika kwa pande zote.
- Ni bora kuondoka kwa heshima na maridhiano kuliko kushikilia madaraka hadi hali iwe tete na kuishia kubeba aibu isiyo ya lazima.
- Rais Biden mara nyingi alitoa ishara kwamba yupo tayari kuweka mbele maslahi ya taifa na familia yake, kuliko kushikilia madaraka kwa nguvu.
- Rais Samia unaweza kufanya vivyo hivyo, kwa kuzingatia afya yako ya kiakili na faraja ya familia yako- Mume, watoto na wajukuu zako ambao wanakutegemea, watafarijika wakikuona ukiwa na amani.
- Kama rais mstaafu, utaendelea kulipwa pensheni yako, kuheshimiwa na kulindwa na taasisi za nchi.
- Kwa hiyo huna haja ya kuendelea kuvumilia presha ya kisiasa inayoweza kukuchosha kimawazo na kukupunguzia furaha ya maisha.
- Ukichukua hatua sasa, utaondoka madarakani ukiwa bado una hadhi kubwa na unapendwa na sehemu kubwa ya wananchi.
- Hii ni bora kuliko kusubiri hadi hali iwe mbaya, uonekane kulazimika kuondolewa kwa aibu au shinikizo.
- Ukiwa kweli kuna mkakati unaopikwa na baadhi ya makundi ndani ya chama au serikali yakO, ni bora Uwaachie waendelee na Ujitoe kwa heshima.
- Utabaki kuwa rais Uliyependa maridhiano na ustawi wa taifa kuliko maslahi binafsi.